Hatimaye kampuni ya Verizon imefanikiwa kununua kampuni ya Yahoo, katika dili hilo wamiliki wa Yahoo wameondoka na dola za kimarekani bilioni 4.5.
Katika dili hilo Mwanamama Marissa Mayer hata jiunga na Verizon hivyo naye zama zake zimefikia mwisho katika kampuni hiyo.
Yahoo sasa itamilikiwa na kampuni ya Verizon ambayo tayari inamiliki kampuni nyingine ya AOL ambayo inafanana na Yahoo, na kama matokeo ya biashara hii inategemewa wafanyakazi zaidi ya 2000 kutoka Yahoo pamoja na AOL watapoteza kazi zao.
Yahoo ilishindwa kuhimili ushindani kutoka kwa makampuni mengine ya barua pepe hasa Google ambao tangu kuja wamekuwa wakiteka soko la matangazo na hivyo kuipa hali ngumu Yahoo. Yahoo walijitahidi kuokoa jahazi kwa kufanya mambo mbalimbali pamoja na kumchukua Marissa Mayer ambaye alikua Google, lakini jitihada zote ziligonga na ndipo walipoamua kuiuza kampuni hii.
Kwa watumiaji wa Yahoo hakuna la kuhofia kwasababu hakutakuwa na mabadiliko kwa sasa, barua pepe na mengine yataendelea vilevile katika anuani zilezile.
Maamuzi ya kuuzwa kampuni hii kwa Verizoni yalifikiwa miezi kazaa nyuma lakini ilikuwa inasubiriwa tu wanahisa wa kampuni hii watoe idhini ya kuuzwa. Yahoo itaendelea kubakia katika soko la hisa mpaka siku ya ijumaa ambapo safari yake ya miaka 21.