Headphones zalipuka, nini sababu ya kulipuka? #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Headphones zalipuka, nini sababu ya kulipuka? #Teknolojia

0
Sambaza

Headphones ambazo ni maarufu kwa kutokuwa bugdha kwa wengine kutokana muundo wake hivi karibuni zilileta maafa kidogo huko nchini Australia wakati mwanamama amoja akiwa safarini.

go to site

Kifaa cha kusikilizia sauti kwenye simu na mitambo mingine ya kompyuta, maarufu kama headphones zilizokuwa zinatumiwa na abiria mmoja zililipuka. go Mwanamke huyo alikuwa amelala akiwa kwenye ndege iliyokuwa safarini kutoka Beijing hadi Melbourne pale alipozinduliwa na mlipuko mkubwa.

Mlipuko wa headphone hizo ulimwacha akiwa na masizi usoni pamoja na malengelenge yaliyotokana na moto kwenye vidole vyake. Headphones hizo ni zile zinazotumia teknolojia ya bluetooth na hivyo ni za kuchaji.

Madhara baada ya kulipukiwa na headphones ambazo betri zake ndio zilikuwa chazo cha mlipuko huo.

Nini chanzo?

Inaaminika kuwa chanzo cha headphones hizo ambazo zilikuwa zikitumia betri ulisababishwa na kasoro kwenye betri za lithium-ion zinazotumiwa katika headphones hizo. Kumetokea visa kadha vya vifaa vyenye betri za lithium kulipuka na kushika moto zkiwemo  simu aina ya Samsung Note 7 jambo lililosababisha simu hizo kuondolewa sokoni.

http://artistestone.com/collection/ares/ Kitendo cha headphones hizo kulipuka zilifanya abiria wakohoe na kubanwa pumzi kwa safari nzima kutokana na moshi uliokuwa umesambaa ndege nzima. Kitendo cha vifaa vya kielektroniki kulipuka imesababisha mashirika mengi ya ndege kutobeba simu aina ya Samsung Galaxy Note 7.

INAYOHUSIANA  Betri la Samsung Galaxy Note 9 ni salama

Headphone hizo hazikuweza kuwekwa wazi na kutambuliwa zilitengenezwa na kampuni gani kutokana na kuaminika kuwa makosa yalikuwa kwenye betri na si headphones. Ni muhimu kuwa makini na kifaa chocote cha kielektroniki.

Vyanzo:  NYDailyNews, NBC news, BBC

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.