Kundi la watafiti kwenye chuo kikuu cha Ben Gurion nchini Israeli wamegundua ya kwamba headphone zinazotumika kwenye kompyuta au simu zetu zinaweza dukuliwa na kutumika kama kinasa sauti(mic).
Hii inamaanisha mdukuzi anaweza akawa akarekodi mazungumzo yanayosikika na ni kwa hadi umbali wa takribani mita 6 kutoka eneo lenye spika.
Programu/app waliyotengeneza wameipa jina la ‘Speake(a)r, programu hiyo ikiwekwa kwenye simu au kompyuta ya mtu inaweza kugeuza mfumo wa spika na kuwa kinasa sauti (mic) na hivyo kurekodi na kisha kuwa na uwezo wa kuyatuma maongezi hayo kwa njia za kimtandao.
Hadi sasa kundi hilo la kiutafiti limeonesha uwezo huo kwa kompyuta tuu, tena zinazotumia mfumo wa teknolojia wa sauti wa RealTek audio – ndio nyingi zaidi. Wamesema kufanikisha jambo hilo kwenye tableti, simu na vifaa vingine vinavyotumia teknolojia ya audio jack inawezekana.
🙂 Kwa sasa watumiaji wenye wasiwasi wa teknolojia ya udukuzi wa namna hii kutumika dhidi yao hawana budi kuchomea vifaa vyao vya ‘audio jack’ – headphones n.k pale ambapo hawavitumii.
Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus
Vyanzo: Wired na mitandao mbalimbali