Helikopta inayotengenezwa Tanzania kuruka 2018

0
Sambaza

Inakadiriwa kwamba ifikapo 2018 Tanzania itakuwa na Helikopta ambayo imetengenezwa hapa hapa nyumbani, ndege hii inatengezwa katika chuo cha ufundi Arusha ambapo ni mabingwa wa kuunda vifaa mbali mbali vya moto.

 

Helikopta inayotengenezwa Tanzania

Picha ya aina ya helikopta kama ambayo chuo cha ufundi Arusha kinatengeneza

Gazeti la kiingereza la Daily News likiripoti habari hii limesema kwamba hatua za mwazo za mradi huu zimekwisha kamilika ikiwamo michoro na mambo mengine ya kibunifu. Kukamilika kwa Helikopta hii kutafungua njia kwa uzalishwaji wa ndege nyingine nyingi za kama hii kwani hii ndiyo kama mfano.

SOMA PIA:  Nokia Kuingia Ushirika Na Zeiss (Watengenezaji Wa Lenzi Za Kamera)!

Akimuelezea Katibu mkuu wa wizara ya elimu Muhandisi Abdi Mjema ambaye ndiye anayeongoza mradi huo amesema kwamba wanashamirisha sera ya viwanda ya Raisi John Magufuli kwa kuleta Helikopta ya kwanza iliyotengenezwa hapa nyumbani.

Ingawa kwa kiasi kikubwa kazi imekwisha kamilika lakini bado timu ya wahandisi hao inawasiliana na mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania kwaajiri ya kupata ruhusa ya kufanyia majaribio ndege hiyo.

helikopta

Aina nyingine ya helikopta ndogo

Timu ya wahandisi ambao wanaifanyia kazi ndege hiyo ni pamoja na muhandisi Abdi mjema na muhandisi Adisai Msongole. Ingawa bado ni mapema mno kujua ni kwa kiasi gani mafanikio ya mradi huu yatahamasisha ukuaji wa teknolojia lakini Teknokona tunajiunga na wadau wengine kuwatakia kila la kheri wahandisi hawa ili waweze kufanikiwa.

SOMA PIA:  Pixelbook: Kompyuta ya kwanza kutoka Google yenye 'Kisaidizi binafsi'

Tupe maoni yako juu ya habari  hiii na pia kama una swali ama maoni usisite kutuandikia.

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com