Hii ndio simu ya Nokia 3310 katika upya wake mwaka 2017! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Hii ndio simu ya Nokia 3310 katika upya wake mwaka 2017!

0
Sambaza

Nokia 3310 ni moja ya toleo maarufu zaidi la simu za Nokia katika miaka mingi iliyopita na sasa imerudishwa -mabadiliko yapo kidogo lakini ni Nokia 3310 ile ile.

http://lostdauphins.com/category/blog/ here Toleo la kwanza la Nokia 3310 lilotoka mwezi Septemba mwaka 2000 liliuzika sana, simu takribani milioni 126 za Nokia 3310 ziliuzika.

go to link Kampuni ya HMD ambayo ina ubia na kampuni ya Nokia katika utengenezaji wa simu zinazobeba jina la Nokia limetambulisha rasmi toleo jipya la Nokia 3310 itakayoanza kupatikana kuanzia mwezi wa nne kwa bei ya takribani Tsh 100,000/=

nokia 3310

Nokia 3310

Nani wamelengwa?

Simu hii ni kwa ajili ya mtu yeyote anayeitaji simu ya ziada yenye uwezo wa kudumu na chaji muda mrefu. Pia ni kwa ajili ya mtu yeyote ambayo anaitaji simu inayofanya kazi muda mrefu bila kuitaji kuchaji na bila kuwa na usumbufu wa apps nyingi hali ambayo ipo kwa simu zingine janja za siku hizi.

INAYOHUSIANA  Facebook katika ulimwengu wa mahaba

Sifa zake

  • Programu endeshaji: Nokia Series 30
  • Display: QVGA inchi 2.4
  • Kamera ya megapixel 2
  • Eneo la kuweka memori kadi (MicroSD) ya hadi GB 32
  • Laini: Kuna toleo la laini mbili na la laini moja
  • Chanja ya Micro USB na uwezo wa Bluetooth 3.0
  • Uzito wa gramu 79.6
  • Opera Mini Browser: Kwa ajili ya kutumia intaneti
  • Gemu: La nyoka, maarufu kwa jina la Snake
  • Pia inakuja na uwezo wa kucheza mziki mafaili ya MP3

Kama sifa ya toleo mama la simu hiyo, toleo hili jipya nalo linauwezo wa kukaa na chaji muda mrefu sana. Ikiwa imeweshwa ila bila matumizi chaji itakaa kwa siku 31, wakati ikiwa hewani tuu (yaani kwenye mazungumzo ya bila kukata simu) basi itadumu masaa 22.

INAYOHUSIANA  VPN ni nini? Fahamu app 3 za bure za Huduma ya VPN

Kama mtu akiitumia kuisikilizia muziki tuu (MP3) chaji itaweza kuhimili hadi masaa 51 ya kusikiliza muziki.

Vipi unamtazamo gani juu ya toleo hili jipya la Nokia 3310? Tuambie kwenye comment.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.