Simu za Nokia ambazo zinaendeshwa na programu endeshaji ya Android zinaendelea kupendwa na kwa sehemu zingine kama Uchina zimejichukulia umaarufu mkubwa.
Matoleo mengi ya Nokia yapo madukani lakini Nokia 6 ambayo ilizinduliwa huko Uchina na kuacha historia ambayo itakumbukwa kwa miaka mingi tu na kampuni husika, soma zaidi hapa.
Hii ni Nokia 7 na ina haya yafuatayo:-
Kioo & Kamera. Kioo chenye ukubwa wa inchi 5.2, ubora wa picha ukiwa 1080*1920 pixels lakini ikiwa inakingwa Corning Gorilla Glass 3 isipate madhara inapoanguka. Upande wa kamera ya nyuma ina MP 16 na ile ya mbele ina MP 5 iliyotengenezwa na Zeiss ikiwa na LED flash mbili.
Programu endeshi & Prosesa. Imewekwa Android 7.1 lakini ikiwa na uwezo wa kuhamia Android 8 (Oreo). Prosesa ambayo ipo kwenye Nokia 7 ile maarufu na inayotumiwa na makampuni mengi tu, Qualcomm SDM630 Snapdragon 630 kasi yake ikiwa Octa-core 2.2 GHz.
RAM & Diski uhifadhi. Moja ya kiungo muhimu cha kufanya simu kutokwamakwama ni RAM, Nokia 7 ina GB 4 na GB 64 uhifadhi wa ndani kwenye simu lakini ikiwa na uwezo wa kukubali uhifadhi wa ziada wa mpaka GB 256.
Betri & Sifa nyinginezo. Hapa kuna betri yenye 3000 mAh aina ya Li-ion ambalo halitoki; linadumu kwa chaji saa 340 ukitumia kwenye intateti tu, saa 15 (kuongea+intaneti), saa 85 ukitumia kusikiliza muziki peke yake.
Nokia 7 ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole iliyowekwa upande wa nyuma, kuna redio, WLAN, Bluetooth, sehemu ya kuchomekea spika za masikioni, GPS, NFC.
Nokia 7 ipo madukani muda mrefu tu na kwa makadirio ni zaidi ya Tsh. 655,00. Nokia 7 Plus, 7.1, 7.1 Plus zipo na zinawika kweli. Uchambuzi wake utakuja katika siku za usoni.
Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360
One Comment
Comments are closed.