Simu za Google Pixels: Hisa za ALPHABET zafunja rekodi ya bei

Hisa za ALPHABET zafunja rekodi ya bei kutokana na Simu za Google Pixels

0
Sambaza

Siku chache tuu zilizopita Google wametambulisha simu janja zao za kiwango cha juu – Simu za Google Pixels, zimepata sifa sana na ALPHABET inanufaika.

Kampuni ya ALPHABET GOOGLE

Kampuni ya ALPHABET: Fahamu makampuni yaliyo chini yake

Jumanne hii hisa za kampuni mama ya Google, ALPHABET zilipanda na kufikia kiwango cha juu kabisa kuwahi kufikiwa tokea mwaka 2014 ambapo hisa za Google zilianza kuuzwa rasmi.

Soma Pia – http://marcinsonpress.com/?wordfence_logHuman=1 ALPHABET: Kampuni ya Google Yafanyiwa Mabadiliko

Jumanne hisa za ALPHABET zilipanda bei kwa http://gunblog.deadcenterfirearmsllc.com/ takribani asilimia 2.5 kufikia bei ya dola za kimarekani 826.85 mchana jijini New York.  Ila mapema siku hiyo pia hisa hizo zilifika hadi bei ya dola 828/hisa, hii ni bei kubwa zaidi kuwahi kufikiwa kwa hisa za ALPHABET – watch tokea Agosti, 2014 hisa hizo zilipoanza kupatikana chini ya jina la Google hazijawahi kufikia kiwango hicho cha bei.

Mafanikio hayo katika mate wake wa hisa yanaletwa hasa na mpokeo mzuri wa simu za Google mpya zinazofahamika kwa jina la Google Pixels.

Simu za Google Pixels zimeshapewa sifa ya kuwa simu bora zaidi za Android zilizotoka hadi sasa na pia zimepewa nafasi kubwa ya kuisumbua Apple na simu zake za iPhone.

simu za google pixel

Muonekano wa matoleo yote ya simu za Google Pixel

Google wamehakikishia watu ya kwamba wataendelea kutoa matoleo ya simu za Google Pixels kila mwaka, na kuzidi kusimamia mfumo mzima wa utengenezaji wa simu hizo na kuzipatia masasisho (updates) ya Android kwa wakati – moja kwa moja kupitia intaneti. Kwa kiasi kikubwa hivi ndivyo Apple wanavyofanya katika biashara ya simu zao za iPhone.

Je bado haujazifahamu simu za Google Pixel? Soma hapa – Google watambulisha simu mpya, zifahamu Google Pixels

INAYOHUSIANA  Google ina kifaa chake cha kudhibiti udukuzi

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.