Hola: Fungua Mitandao Inayozuiwa Kufunguka Tanzania

0
Sambaza

Hola-Unblocker-tanzaniaLeo tutakueleza jinsi ya kuweza kufungua mitandao maarufu ambayo inaweza kufunguka/kutumika kwa watu waliokatika nchi flani tu. Hii mara nyingi inakuwa katika mitandao ambayo baadhi ya huduma zao kama vile  muziki au video wanajikuta wamebanwa kisheria au kimikatika kuonesha data/huduma husika kwa nchi zingine.

Je umeshakutana na ukurasa wa mtandao unasema kitu kama hiki?

Alama inayoonesha huduma ya mtandao husika haupatikani katika nchi husika

Alama inayoonesha huduma ya mtandao husika haupatikani katika nchi husika

Pia suala hili linaweza kuja ata pale unapotaka kuangalia baadhi ya video katika akaunti ya YouTube;

SOMA PIA:  Apigwa faini milioni 9 kwa kubonyeza kitufe cha 'Like' facebook

teknokona-tanzania-mtandao

Njia rahisi ya kushinda suala hili ni kupitia kutumia programu moja inayeweza kufanya kazi kama kiprogramu cha nyongeza (extensions/plugins) kwenye Chrome au Firefox inayofahamika kwa jina la Hola. Programu hii inapatikana pia kwenye Android na itakuwezesha kutumia apps zinazonyima baadhi ya huduma zake kwa watu walio katika nchi flani.

Kwa ufupi Hola itakupa uwezo wa wewe kuchagua unataka kutambulika kama mtumiaji kutoka nchi gani, utaweza kuchagua na kubadilisha kwenda nchi yeyote utakayoitaka yote ni ili kukuwezesha kuweza kupata huduma husika.

SOMA PIA:  Facebook kufundishwa kama kipengele katika somo la Kiingereza nchini India

hola-unblocker

Kwenye Android utafungua app hiyo na kuchagua app unayotaka idanganya uhalisia wa nchi uliyopo, kisha ndiyo utafukua app husika.

Kupakua bofya sehemu husika Android | Chrome | Kwa ajili ya iOS, Windows, Firefox na Mac <Bofya Hapa>

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com