HP yatoa printer ndogo inayoenea kwenye kiganja cha mkono #Teknolojia

0
Sambaza

Urahisi wa kubeba vitu siku hizi ndio makampuni mengi duniani yanachozingatia ili kumfanya yule mtumiaji asichukie kile kifaa alichokinunua kwa fedha nyingi. HP sasa imeamua kuleta printer ndogo inayoweza kubebeka kiurahisi sana.

Sasa kama ulikuwa unatumia fedha nyingi kutoa nakala ya picha ndogo basi ni muhimu ukanunua HP Sprocket ili kuweza kuondokana na adha ya kutumia fedha nyingi wakati ambapo kifaa hicho kinakuwezesha kutoa nakala ya picha ndogo wakati wowote na sehemu yoyote.

Mfano wa nakala ya picha iliyotoka kwenye HP Sprocket.

Uwezo, muonekano na upatikanaji wa HP Sprocket (Sifa za HP Sprocket).

Kifaa hiki cha kutoa nakala ya picha kwenye karatasi maalum kina uzito wa gramu 172 na upana wa 116 x 75 x 23mm. Kina sehemu moja ya kuchomomekea USB ndogo pamoja kitufe cha kuwasha/kuzima kifaa husika. Ina makaratasi 10 ya aina ya Zink ambayo ndio yanatumika kutoa nakala ya picha ndogo pana (kubwa kidogo kuliko passport size). 

HP sprocket ina taa 2 za LED; ya upande wa kulia inatoa mwanga mweupe kama ishara ya printer imeunganishwa vizuri huku taa ya upande wa kushoto inaashiria kiasi cha chaji.

Usiwaze kuhusu muda inayottumia kujaa chaji, inachukua dakika 90 kujaa chaji na ina teknolojia ya Bluetooth 3.0 pamoja na NFC kwa mantiki hiyo inafanya kazi kwa kutumia app yake tu inayopatikana kwenye Android na iOS.

Mbali na kuwa na karatasi 10 za aina ya Zink; HP Sprocket ina karatasi moja ya ziada inayoitwa Smartsheet ambayo katika kila kifurushi cha makaratasi smartsheet inakaa chini kabisa ya karatasi zote ikiwa kazi yake ni kusafisha uso wa juu wa printer kabla nakala hazijaanza kutolewa. Pia kazi yake ni kuhakikisha hakina hata karatasi moja iliyowekwa kwenye printer itoke bila kutumika.

SOMA PIA:  Satelaiti ndogo zaidi yaundwa nchini India

Nakala ya picha zinazotoka kwenye HP Sprocket zinaweza kutumika kama stickers, yaani unaweza ukazibandika sehemu bila kuhitaji gundi ya aina yoyote ile

App ya HP Sprocket inayoweza kutoa nakala ya picha katika mfumo wa JPEG, GIF, PNG, BMP, PNG, TIFF kutoka kwenye simu (gallery) au kutoka kwenye mitandao ya kijamii. \pia, inawezekana kupiga picha papo kwa papo na ukatoa nakala yako.

 Bei yake ni $139|Tsh. 312,611 ikija pamoja na karatasi kumi za Zink na karatasi hizo zinauzwa kwa $8|Tsh. 17,992 (kwa kifurushi cha karatasi 20). HP Srocket imeanza kuuzwa tangu mwezi uliopita nchini India ila inawezekana kuagiza kupitia Amazon.

Chamzo: Gadgets 360

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com