HTC 10: Toleo jipya la simu janja kutoka HTC! #Uchambuzi

2
Sambaza

Jana Jumanne, tarehe 12 Aprili 2016, Kampuni ya HTC ilizindua simu janja yake mpya iliyopewa jina la HTC 10 kwenye soko, Jina la HTC 10 limetokana na kuenzi miaka kumi ya kampuni ya ki-Vietnam tangu ianze kutengeneza simu janja zake yenyewe.Imekua safari yenye kuvutia kuona HTC na mikakati ya bidhaa zake kwa kipindi cha miaka kadhaa huku Apple na Samsung wakitawala eneo kubwa la soko na mawazo ya watumiaji.

Sifa Zake

Utofauti mkuu wa simu hii mpya ya HTC   upo kwenye mfumo wa kamera na sauti (audio). Kampuni ya HTC ina historia ndefu ya kufikri kwa makini kuhusu mifumo ya sauti (audio) kwenye simu zake. Ikumbukwe washawahi kuwa na ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Beats. Kampuni imeweka spika mbili, moja iliyopo mbele ya simu karibu na kamera ya mbele na nyingine ipo chini ya simu. Pia wameongeza ufanisi kwenye sauti kupitia headphones.

SOMA PIA:  Kipengele cha "Private Reply" kiliwekwa kimakosa (kutoka kabla ya muda wake)

_htc-10-hands-on-13.0

HTC pia wanatumia nguvu ya ziada kuitangaza kamera yao megapixel 12, huku wakidai “Inawezekana ni kamera bora ya simu janja iliyopo sokoni leo”. Madai hayo yatahitajika kusubiri uchunguzi, lakini pia kamera ya HTC 10 imeweka programu inayofanya ‘image-stabilization’ kwenye kamera zake zote mbili ya mbele na nyuma. HTC pia imedai kamera yao ina uwezo wa kufanya vizuri hata kwenye mwanga hafifu na ina uwezo wa kuchukua video za ubora wa 4K.

SOMA PIA:  Google AutoDraw: Sasa hivi mtu yeyote anaweza kuwa mchoraji mzuri

Hardware/Sifa za Kiundani

Simu hii yenye inchi 5.2 ina processor ya hali ya juu kama processor zinazotumika na wapinzani wao, kama vile Samsung Galaxy S7 Edge, na ina ram GB 4. Pia inakuja na ujazo (storage) wa  GB 32 na ina uwezo wa kuongeza ujazo hadi kufikia TB 2 (Memori kadi/SD Card). HTC pia inadai uhai wa betri ya HTC 10 unaweza kudumu hadi siku 2 ukiichage mara moja.

Kwenye upande wa screen HTC wanatumia screen inaoitwa “Super LED” ikiwa imefunikiwa na kioo kinachoitwa “Gorilla Glass” kwa ajili ya usalama zaidi. Pia ina ‘finger print reader’ kwa sababu za kiusalama kwa ajili ya mtumiaji wa simu.

htc 10

Programu endeshaji

HTC 10 zinakuja na mfumo wa Android Mashmallows, toleo jipya kabisa la operating system kutoka Google. Pia HTC wamechukua hatua ya kupunguza application zinazokuja zikiwa zimasanikishwa kwenye simu (pre-installed).

SOMA PIA:  Youtube yazidi kuwawekea ngumu wenye msimamo mkali

Pia muonekano wake umebadilishwa kumuwezesha mtumiaji kuweza kubadili mpangilio wa programu zitakvyoonekana kwenye menu kuu jinsi anavyoona inafaa kwa matumizi yake.

htc 10

Sifa zingine kwa undani

RAM – GB 4 | Kemera 12 Ultrapixel | Kamera ya selfi – 5 Megapixel | Betri mAh 3000 | Diski uhifadhi – GB 32

htc10b

Vyanzo :NDTV

Picha : The Verge, NDTV

HTC 10 itaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi Mei na bei inategemewa kucheza kwenye dola 699 za kimarekani (takribani Tsh 1,529,000/= | Kes 70,700). Tuambie mtazamo wako kupitia eneo la comment.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.
error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com