HTC kutoa simu (bidhaa mpya) mwishoni mwa mwezi Mei - TeknoKona Teknolojia Tanzania

HTC kutoa simu (bidhaa mpya) mwishoni mwa mwezi Mei

1
Sambaza

HTC hawapo mbali sana kuleta kitu kizuri mbele ya wateja wake duniani kote kwani baada ya uvumi kuenea kuwa watatoa simu janja mpya mwezi Mei sasa wameweka wazi kabisa tarehe ambayo uzindizi utafanyika.

Imekuwa kama desturi ya makampuni mbalimbali kuendelea kutoa simu rununu ambazo zinatoka katika “Familia” moja kama wamavyofanya Apple, Samsung, Xiomi, n.k HTC nao wameona sasa ni wakati sahihi wakutoa HTC U12+.

mwishoni mwa mwezi Mei

HTC U12+ simu rununu ambayo itakumbana na OnePlus 6 kwenye soko kwani nayo itazinduliwa siku hiyohiyo.

HTC U12+ itazinduliwa Mei 23 2018 na kama ilivyo kawaida ya makampuni mengi kutoa bidhaa zaidi ya moja katika siku husika, pengine HTC wakazindua pia HTC U12 ingawa hakuna uhakika kuhusiana kuzinduliwa kwa simu hiyo (HTC U12) katika tarehe iliyotangazwa.

mwishoni mwa mwezi Mei

Tarehe rasmi ambayo simu janja, HTC U12+ itazinduliwa.

Simu janaja, HTC U12+ ni simu inayoelezewa kuwa ni zaidi ya “Sifa zake” kwa sababu ya vile ambavyo simu hiyo imetengenezwa ili kuifanya HTC iwepo katika ramani nzuri ya kimauzo ya bidhaa zake. Sifa za HTC U12+ ni kama ifuatavyo:-

INAYOHUSIANA  Ujio wa HTC U12 Life haupo mbali sana

buy clomid and nolvadex online Prosesa: Qualcomm Snapdragon 845 SoC

http://walanet.org/members-only/meeting-minutes/ Kioo: Kioo chake ni cha LCD chenye ubora wa QHD+ na ukubwa wa inchi 5.99 katika uwiano wa 18:9

do i need a prescription to buy flagyl Kamera: Ina kamera mbili, mbele na nyuma; kamera ya mbele ina MP 8 kila moja za zile za nyuma zina MP 12 kila moja

Programu endeshi: Oreo

RAM/Diski uhifadhi: Ina RAM GB 6, diski uhifadhi wa GB 64/128

Betri: 3420mAh na betri yake haitoki (ni ya ndani kwa ndani)

mwishoni mwa mwezi Mei

Kwenye HTC U12+ utaweza kubinya kwa pembeni ili kuweza kupiga picha, kuanza kutumia Google Assistant.

Bei yake bado haijawekwa wazi hivyo tusubiri mpaka siku itakayozinduliwa na kwa hakika TeknoKona tutawataarifu mengi zaidi kuhusiana na uzinduzi wa HTC U12+.

Vyanzo: GAdgets 360, EveningStandard

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|