HTC Kuuza Sehemu ya kampuni au kampuni yake Yote – Inajitafakari!

0
Sambaza

Kwa mujibu wa Bloomberg, kampuni ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki zikiwemo simu za mkononi ya HTC inatarajia kuuza sehemu au biashara yake yote.

Kampuni ya HTC imejijengea umaarufu mkubwa kwa kutengeneza simu janja (Smartphones) kwa miaka kadhaa iliyopita.

Kutokana na kukua kwa ushindani kutoka kwa Samsung na Apple, kampuni ya HTC imeshindwa kujihakikishia msingi imara wa wateja hivyo kuamua kujiingiza katika ubia.

Kampuni hii pia ilipoteza maafisa wake muhimu miaka kadhaa iliyopita, akiwemo Mkurugenzi wake mkuu Peter Chou, ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Cher Wang mnamo mwaka 2015.

Toleo la karibuni la simu za HTC ni HTC U11 ambayo imeuzwa kwa kiasi kidogo sana huko nchini Marekani.

Simu ya HTC-U11 HTC Kuuza kwa Sehemu au Kampuni yake Yote

HTC Kuuza kwa Sehemu au Kampuni yake Yote: Soko la bidhaa za simu limezidi kuwa na ushindani sana miaka hii

HTC inalenga kuuza pia biashara yake ya uhalisia onyeshi (Visual Reality) ambayo kwa mujibu wa Bloomberng iliianzishwa kwa msaada wa kampuni ya Valve. Mfumo huo onyeshi wa HTC unaojulikana kama Vive unashindana vikali na ule wa Facebook wa Oculus. Hivi karibuni HTC wamepunguza bei ya bidhaa yao hii kwa bei ya dola 200 ili kuvutia wateja.

Soma pia: iPhone 6, Samsung Galaxy S6 Au Htc One M9: Simu Ipi Rahisi Kutengeneza Ikiharibika?

SOMA PIA:  Kipengele cha "Private Reply" kiliwekwa kimakosa (kutoka kabla ya muda wake)

Hata hivyo msemaji wa HTC alipohojiwa na chombo cha habari cha CNBC, hakuwa tayari kuzungumzia swala hilo.

Je wewe ni mtumiaji wa simu na vifaa vya HTC? Je bado unaamini na kukubali bidhaa za HTC? Tafadhali tuandikie maoni kisha washirikishe wengine.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Kornel ni mfuasi mkubwa wa maswala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Ana uzoefu mzuri katika maswala mbalimbali yanayohusu kompyuta na teknolojia. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali kama vile kutengeneza tovuti, kutengeneza programu mbalimbali, usanifu picha na video bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com