HTC ONE: Simu Yenye Mvuto Na Uwezo Wa Hali Ya Juu! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

HTC ONE: Simu Yenye Mvuto Na Uwezo Wa Hali Ya Juu!

0
Sambaza

buy lexapro online ireland  

Baada ya kuwa na mwaka mbovu kimapato kampuni ya HTC imeibuka na simu ya kipekee.

 

Kampuni ya HTC ni kampuni inayokubalika sana kwa upande wa ubunifu lakini imekuwa inajikuta bidhaa zake hazifanyi vizuri sokoni kulinganisha na bidhaa za Apple na Samsung. Tofauti kubwa imeonekana HTC hawajawa wakiweka fungu kubwa la pesa katika kuzitangaza bidhaa zake kama washindani wake wafanyavyo, hivyo kufanikiwa kwa HTC ONE kutategemea sana jinsi gani kwa wakati huu watajikita katika kuitangaza.

Dilantin without a prescription

Ubunifu wa HTC ONE (M7) ni wa hali ya juu na uwezo wake ni mkubwa sana kulinganisha na simu zingine zote zilizopo sokoni kwa sasa.
 
Baadhi ya uwezo wa kipekee ni pamoja na kuwa na spika mbili za stereo pamoja na amplifaya na hivyo kutoa sauti yenye kiwango cha juu. Pia kwa wale wenye ‘Smart TVs’ basi ukiwa na HTC ONE huitaji kubeba rimoti kila saa, HTC ONE inaweza kutumika kama rimoti. Kingine zaidi ni kamera yenye uwezo mkubwa sana, utakapo’click’ basi kamera hiyo itapiga picha 20 na video ya sekunde 3 kwa mara moja-vyote vitafanyika kwa wakati mmoja ndani ya sekunde 3. 
 
HTC ONE inatumia programu ya uendeshaji ya Android 4.1 (Jelly Bean).

buy inderal for anxiety

  • Kioo cha inchi 4.7 HD (1920 x 1080 pixels)
  •  Prosesa -Quad core Qualcomm Snapdragon, 1.7GHz
  • RAM 2GB
  • Ukubwa Uhifadhi wa GB 32 au 64
  • Bluetooth 4.0
  • WiFi, DLNA, 4G LTE, DLNA
  •  microUSB port na 3.5mm audio jack

Inatarajiwa kuingizwa sokoni kwenye masoko masoko mbalimbali kuanzia mwisho wa mwezi huu, kuhusu suala la bei itakubidi kutayarisha si chini ya shillingi milioni moja na laki mbili za kitanzania (1,200,000/=).

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung kuzindua memori kadi ya 512GB
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply