Huawei Katika Mchakato Wa Kutoa Simu Nyingine Ya Toleo La Honor! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Huawei Katika Mchakato Wa Kutoa Simu Nyingine Ya Toleo La Honor!

1
Sambaza

Huawei ni kampuni ya tatu kwa ukubwa katika maswala ya kutengeneza simu duniani. Kwa sasa ndio kampuni kubwa ambayo inaongozwa kuwa mshindani wa simu za Apple na Samsung.

Toleo lake lililopita katika mfululizo wa Honor lilikuwa ni Huawei Honor 8 na kwa sasa ina ripotiwa kwamba kuna toleo linguine la Honor ambalo lipo njiani.

Huawei

Ukiachana na kesi ambazo ziliwakumba wakuu wa Huawei kuhusu kuvujisha siri za kampuni bado kampuni hilo limejikita katika kuhakikisha kuwa inawapa wateja wake kile ambacho wanakitaka.

Ripoti hizi bado hazijaweka wazi juu ya jina la simu hiyo (lakini injulikana kuwa ni katika muendelezo ule wa Honor) hivyo basi inaweza ikawa ni huawei Honor 9.

INAYOHUSIANA  Miaka kumi ya App Store kwenye biashara

FUNUNU JUU YA SIFA
facebook – Prosesa ya octa-core ya 2.4 GHZ yenye CPU ya Kirin 960
where can i buy finast pills – Display ya inchi 5.7 ya kioo cha Quad HD
http://mykrumlov.com/category/activities-attractions-cesky-krumlov/page/2/ – RAM ya GB 6
– Ujazo wa uhifadhi wa GB 128
– Betri ya uwezo wa mAh 3900
– Simu itakuwa na uwezo wa laini mbili
– Inasemekana kuwa itakuja na kamera mbili pia
– Uwezo wa kamera ni Mp 12 kwa kamera ya nyuma na kamera ya mbele ikiwa na Mp 8
– Ina uwezo wa 4G LTE na uwezo wa 4.1
– Itakuja katika rangi ya Gold wakati wa kuzinduliwa

Baada ya kusema hayo hatuna budi kuisubiria simu hii tuone kama sifa na jina vitaendana na fununu ambazo zipo mtaani kwa sasa?

Huawei

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment je ni toleo la simu gani ambalo unalisubiria kwa hamu? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

INAYOHUSIANA  Taka zinazotokana na bidhaa za simu ni kero

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com