Huawei Nova; Fahamu kuhusu simu mbili mpya kutoka Huawei

0
Sambaza

Huawei wametambulisha simu mbili hapo jana, Huawei Nova, na Huawei Nova plus. Simu hizi zinaonekana kuja kuleta ushindani katika soko la simu za bei ya kati, na pia kuzidi kukuza nafasi ya Huawei katika soko la simu duniani.

huawei nova

Muonekano

Kama majina yake ya yalivyo, ukitoa tofauti kadhaa baina ya simu hizi mbili, ukubwa ni moja ya tofauti kuu.

Hizi ni simu zenye muonekano wa simu za hadhi ya juu (hasa kutokana na kuacha kutumia plastiki),zikiwa pia na uwezo wa ngazi ya kati (mid range).

huawei nova

Muonekano wa nyuma, nyuma kabisa ni Nova Plus na mbele ni Nova.

Sifa za Huawei Nova

  • Ukubwa – inchi 5 (display – 1080p HD)
  • Prosesa ya Snapdragon 625
  • RAM ya GB 3
  • Diski uhifadhi GB 32
  • Kamera ya megapixel 12
  • Kiwango cha betri cha mAh 3,020
  • Bodi ya simu imeundwa kwa kutumia malighafi za alumini (aluminium)

Sifa za Huawei Nova Plus

  • Ukubwa – inchi 5.5,
  • Kamera megapixel 16
  • Betri – mAh 3,340
SOMA PIA:  Maana ya "i" kwenye bidhaa za Apple #Teknolojia

Ukitoa tofauti hizo chache mengine yote yanafanana na uwezo ulio kwa Huawei Nova. Na simu zote zinakuja na toleo la Android 6.

Muonekano wa nyuma wa Nova Plus

Bei

Huawei Nova inategemewa kuuzwa kwa bei ya kati ya Tsh 970,000/= | Ksh 45,000.

Huawei Nova Plus kwenye Tsh 1,050,000/= | Ksh 48500/=... (tegemea chini kidogo au juu kidogo zikianza kupatikana nchini)

Zitafanikiwa?

Inaonekana Huawei wanajikita katika kuhakikisha wanabadilisha mtazamo wa suala la ubora kwa bidhaa zinazotoka nchini China kwa makampuni ya kichina. Huawei tayari kupitia simu zake za familia ya P, Huawei P, wamefanikiwa kuuza vizuri katika masoko ya ulaya na marekani.

SOMA PIA:  Apple Kutengeneza Simu ya Kujikunja Ifikapo 2020, kushirikiana na LG!

Simu hizi zitaanza kupatikana katika nchi mbalimbali kuanzia mwisho wa mwezi huu wa tisa.

Je una mtazamo gani juu ya simu hizi mbili kutoka Huawei?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com