Huduma za TigoPesa na M-Pesa vyapata vyeti vya ubora - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Huduma za TigoPesa na M-Pesa vyapata vyeti vya ubora

2
Sambaza

Miamala kwa njia ya simu ni jambo la kawaida sana katika nchi nyingi tu za Afrika na huduma za M-Pesa na TigoPesa zinazotolewa na Tigo na Vodacom Tanzania zimepewa vyeti kuidhinishwa kuwa huduma bora za kifedha.

HUduma za kifedha zinatumika sana na kuwa ajira kwa wengine, kurahisisha miamala (kutuma/kupokea pesa) na hata kuongea pato la taifa kwa njia ya ulipaji kodi. http://camanual.com/download/statutory-compliance-chart-month-november-2017/index.php?_nonce=a4cea106cf Mwaka 2018 Aprili 13 utaingia kwenye historia ya Tigo na Vodacom Tanzania baada ya huduma ya TigoPesa na M-Pesa kutimiza vigezo vyote kwa asilimia 100 hivyo kutambulika kimataifa kama huduma bora.

Huduma za TigoPesa na M-Pesa

Kuna akunti za kufanya miamala ya kifedha zaidi ya 690 milioni duniani kote jambo linalowezesha watu kuhifadhi pesa zao na kuweza kupata huduma ya kifedha kwa mapana zaidi.

Undani wa TigoPesa na M-Pesa kupewa cheti cha ubora.

Katika kukidhi viwango vya mtoa huduma za kifedha anayetambika na GSMA Mobile Money ni laziam awe amechunguzwa na kuthibitika ni za kuaminika, kuna uwazi na usalama wa fedha za wateja wao. source Vigezo vyote hivyo ni lazima mtoa huduma apate alama 100 katika kila kigezo kilichowekwa na GSMA Mobile Money.

Huduma za TigoPesa na M-Pesa

Tigo na Vodacom ndio mitandao ambayo inaongoza zaidi kwa kufanya miamala ya kifedha kwa njia ya simu. Ukiunganisha wateja wa Tigo na Voda ni karibu ya nusu ya wateja mitandao ya simu wote nchini Tanzania.

Makampuni mengine yaliyopata cheti cha ubora kutoka GSMA Mobile Money ni pamoja na source link Orange Côte d’Ivoire, Safaricom (Kenya) na Telenor Microfinance Bank Ltd. (Easypaisa Pakistan).

Kwa uthibititsho huu unaziweka TIgoPesa na M-Pesa katika nafasi nzuri kuzidi kuaminiwa na wateja wake na pengine hata kuleta mengi mazuri kwa wateja wa huduma hizo.

Vyanzo: TIgo, Dignited

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|