Hyperloop - Safari ya KM 1000 ndani ya Saa 1, Teknolojia Kufanyiwa Majaribio Mwaka huu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Hyperloop – Safari ya KM 1000 ndani ya Saa 1, Teknolojia Kufanyiwa Majaribio Mwaka huu

0
Sambaza

Tulikwishaandika kuhusu ujio wa teknolojia ya Hyperloop itakayowezesha usafirishati wa mizigo au watu kwa kasi sana, mfano safari ya Dar hadi Arusha kukamilika ndani ya nusu saa tuu. Mwaka huu teknolojia hiyo itafanyiwa majaribio rasmi.

Kampuni inayosimamia mradi wa teknolojia hiyo, Hyperloop Technologies tayari imeonesha maandalizi waliyofikia kuhakikisha ndani ya mwaka huu wanajenga mfumo huo wa usafiri huko North Las Vegas, Nevada, kwa kiwango kidogo kwa ajili ya kuwawezesha kufanya majaribio ya teknolojia hiyo.

Mabomba spesheli kwa ajili ya njia ya Hyperloop yakiwa tayari eneo la wazi huko North Las Vegas

Mabomba spesheli kwa ajili ya njia ya Hyperloop yakiwa tayari eneo la wazi huko North Las Vegas

Kupitia mabomba spesheli ya aluminiam yaliyotolewa hewa kabisa (vacuum), chombo spesheli kitaweza kusafiri ndani ya mabomba hayo kwa hadi mwendokasi (speed) wa km 1000 ndani ya lisaa limoja (km 1000/saa).

Kampuni ya Hyperloop Technlogies inampango wa kufikia mwaka 2020 -21 wawe wameshatengeneza mfumo wa usafiri wa kutumia teknolojia ya Hyperloop. Watatumia mfano mdogo wanaoujenga na kukamilisha mwaka huu kama sehemu ya kujifunza zaidi kabla ya kujenga mfumo mkubwa zaidi na wa gharama kubwa.

INAYOHUSIANA  NASA, Uber kuleta usafiri wa anga katika miji yenye watu wengi

http://howdidyouaffordthatcar.com/?author=36 Teknolojia hii ikianza kutumika itawezesha usafirishaji wa watu na mizago kuwa haraka zaidi kuliko chombo chochoto cha usafiri kinachotumika kwa sasa.

Mchoro unaoonesha jinsi wasafiri watakavyoweza kukaa katika chombo hicho cha usafiri

Mchoro unaoonesha jinsi wasafiri watakavyoweza kukaa katika chombo hicho cha usafiri

 

Mchoro ukionesha ubebaji wa kontena la mizigo ndani ya Hyperloop

Mchoro ukionesha ubebaji wa kontena la mizigo ndani ya Hyperloop

021_14A_HYPERLOOP ART

Mabomba spesheli yatakayokuwa njia yataweza kujenga juu au chini ya ardhi na yataweza kuhimili hadi tetemeko la ardhi bila kuharibika.

Ushindani pia umeongezeka baada ya kampuni nyingine kuibuka inayofahamika kwa jina la Hyperloop Transportation Technologies ya Calfornia ambayo imesema ipo katika mipango ya kutengeneza sehemu ya majaribio ya teknolojia hiyo hiyo ndani ya miezi michache inayokuja.

Je una maoni gani juu ya maendeleo haya katika teknolojia? Kufahamu zaidi kuhusu teknolojia hii soma makala yetu iliyopita -> HYPERLOOP: Fikiria Kusafiri Kutoka Dar hadi Arusha ndani ya Nusu Saa Tuu!

Vyanzo: Mitandao ya Engadget, The Verge.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply