Ifahamu Program Endeshaji Mpya Ya Android Baada Ya ‘Android Nougat!

0
Sambaza

Android O ni jina ambalo imepewa programu endeshaji ijayo kutoka Android ambayo inamilikiwa na Google. Kwa maana nyingine hii inaweza ikajulikana kama Android 8.0

Kwa sababu ya sasa inaitwa Android 7.0 au Nougat. Android O kwa haraka haraka ni kwamba itakua na maboresho ya aina yake ukilinganisha na matoleo ya nyuma.

Picha Inayo Onyesha Mwenendo Wa Android O kuanzia katika hatua za mwanzo (Developer Preview -DP- 1 Mpaka 4) Mpaka Muda Wa Kutolewa Rasmi

Kumbuka Android ndio programu endeshaji inayoongoza kutumia zaidi duniani katika simu janja na vifaa vingine.

Inavyosemekana ni kwamba programu endeshaji hii itatolewa rasmi agosti 21, 2017 na hii ni siku chache tuu kutoka sasa.

Muonekano Ambao Umepatikana Katika Toleo La Developer Preview

SIFA ZAKE KWA UCHACHE

  • Maboresho katika eneo la Notification
  • Maboresho katika Background Apps, kwa kudhibiti matumizi
  • Maboresho katika ku’copy na ku’paste
  • Maboresho katika soko la Google Play ambapo utaweza kuweka ‘pause’ update yeyote ile ili kufanya data isitafunwe (kutumika katika zoezi hilo)

Maboresho Kadhaa Katika Eneo La Notification

Ukiachana na hayo kutakua na maboresho mengine kadha wa kadha ambayo tutayaweka wazi programu endeshaji hii ikitoka rasmi

SOMA PIA:  Simu janja 7 kutoka China ambazo hazijulikani na wengi! (2017) #Uchambuzi

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment. Je hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com