Ifahamu ‘Google Hire’ Njia Bora Ya Kupata Wafanyakazi Kwa Kampuni Ndogo Na Za Kati!

0
Sambaza

Google imekuja na njia mpya ambayo inawezesha makampuni kupata wafanyakazi kwa urahisi kabisa. Google Hire inakua inahifadhi taarifa kama zile za mawasikiano, CV na mengine mengi kutoka kwa waombaji wa nafasi za kazi.

Google Hire ni njia rahisi ya kutafuta vipaji (wafanyakazi bora) na vile vile kuweka mahusiano mazuri kati ya mwombaji kazi na mtoaji kazi.

Google Hire

Vile vile Google wanasema kuwa taarifa ambazo mwajiri ataweza kuaziona ni zile tuu ambazo mtafuta ajira atakubali zionyeshwe. Google Hire itafanya kazi na G Suite (amabyo ina vitu kama G maill, Google Callender n.k)

Google Hire

Google Hire Itakuwa Na Mambo Haya.

  • Kuwa na mawasiliano kati ya pande mbili kwa kutumia Gmail au Google Hire.
  • Kupanga ratiba ya mahojiano (interview) na taarifa za mahojiano hayo ndani ya Google Hire
  • Waajiri wanaweza wakajua chimbuko la wafanyakazi wao (Uzoefu wa kazi)  kwa kwa kutumia Google Hire

Google Calendar Kutumika Katika Kupanga Ratiba Ndani Ya Google Hire

Kumbuka ni mwezi wa tano tuu hapo mtandao wa Google ulikuja na Google For Jobs ambayo hii ni msaada mkubwa kwa wale ambao wanatafuta kazi. Hii ni msaada mkubwa kwa wale wanaotafuta kazi na wale wanaotoa kazi hizo.

SOMA PIA:  Kipengele cha 'Smart Battery' kwenye simu za Google Pixels

Google imejitetea na kusema kuwa Hire ina utofauti mkubwa sana na mitandao mingine kama vile LinkedIn kwani Hire inatumia G Suite.

Google Hire Kutumiaka Katika Kutoa Mrejesho (Feedback)

Kama ni mtumiaji mzuri wa G Suite na unatafuta kazi basi huna budi kuingia katika Google Hire .

Ningependa kusikia kutoka kwako niambie hii umeipokeaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment,

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Kila Siku, Kwani TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com