Ifahamu simu ya Moto Z kutoka Lenovo! #Uchambuzi

0
Sambaza

Kila siku kuna simu janja inaingia sokoni kwa ajili ya wateja kutumia lakini pia kukuza teknolojia ambayo inakuwa kwa kasi sana duniani kote. Makala hii inaangazia toleo la Moto Z kutoka Lenovo.

Lenovo ambao ni maarufu kwa utengenezaji wa laptops lakini pia hujihusisha na utengenezaji wa simu. Mwaka jana mwezi wa tisa, Lenovo walitambulisha simu ya Moto Z amabayo inakuja na matoleo mawili; Moto Z na Moto Z Force.

Mojawapo ikiwa na “Shatterproof screen” (mojawapo ya screen protectors), sumaku ambayo itamuwezesha mtumaji kuweka vitu vijulikanavyo kwa ujumla kama “Mods” nyuma ya simu ambayo ni vitu kama vile “Pico projector” kwa ajili ya kuonyesha picha kwenye ukuta, betri ya ziana pamoja na stereo speakers.

Moto Z

Moto Z

Specifications za “Moto Z”

  • inchi 5.5 quad HD AMOLED screen
  • Snapdragon 820 processor (kutoka kampuni ya Qualcomm )
  • GB 4 za RAM,
  • 32GB ya uwezo wa kuhifadhi vitu (storage) pamoja na sehemu ya kuweka memory card,
  • Ubora wa picha 13-megapixels kwenye kamera
  • Uwembamba wa 5.2mm
SOMA PIA:  Apps mbalimbali katika simu moja kwa akaunti mbilimbili

Huku aina ya pili ya simu kutoka Lenovo inaitwa “Moto Z Force” ikiwa na specifications zinazofanana na aina ya kwanza ila yenyewe ina utofauti kidogo:-

  • “ShatterShield screen protection”
  • pia uwembamba wake ni 7.7mm
  • ina betri kubwa zaidi ya betri lililopo kwenye Moto Z
  • pia ubora wa picha kutoka kwenye kamera ni megapixels 21.
Muonekano wa nyuma wa Moto Z Force

Muonekano wa nyuma wa Moto Z Force

Simu hizo zinatarajiwa kuingia sokoni mwezi Septemba na kila moja itagharimu dola 499. Hata hivyo wachangauzi wanasema kuwa ubunifu huo huenda ukawa vigumu kuuza kutokana na kwamba simu janja zote mbili hazina sehemu ya kuchomekea headphones, zikitegemea USB-C port kwa ajili ya kutumia stereo speakers.

Hatua hiyo itaathiri juhudi za Lenovo kuimarisha mauzo yake ya simu pamoja na zile za kitengo cha Motorola ilizonunua kutoka kwa Google kwa takribani dola biloni 2.8 mwaka 2014 kutokana na soko la simu janja kuwa na ushindani mkubwa.

SOMA PIA:  Kaspersky yakiri kupakua nyaraka za siri za Marekani

Una lolote la kusema kuhusu makala hii? Niandikie comment yako nipate kusikia kutoka kwako. Teknokona daima tupo na wewe.

Vyanzo: Know your mobile, motorola-blogspot.com

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com