Ifahamu TV ya 4K Ambayo Inabamba Zaidi Ya HD - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Ifahamu TV ya 4K Ambayo Inabamba Zaidi Ya HD

0
Sambaza

Je unadhani ya kwamba runinga za HD (high Definition ) ndiyo aina ya kisasa zaidi? Pole kama ulidhani hivyo maaana teknolojia imekwisha kuacha, runinga mpya zilizopewa jina la 4k ndiyo teknolojia mpya zaidi kwa huu upande wa runinga. 4k ni aina ya runinga mpya ambazo zimeboreshwa katika mfumo wa uundaji wa picha. Wakati runinga za HD zinaunda picha zake katika saizi (pixels) ya 1080 yaani 1080×1920, mfumo mpya wa runinga wa 4k utaongeza zaidi saizi(pixels) ya picha na hivyo kufanya picha zionekane safi zaidi.

Ulinganishi wa mifumo ya  uundaji wa picha.

Ulinganishi wa mifumo ya uundaji wa picha.

Je teknolojia hii ya 4K inatofauti gani hasa na teknolojia ya HD ambayo ndio inatumika zaidi sasa?

Mfumo huu mpya wa 4K utakuwa unatumia picha zenye saizi (pixels)
Ya 4096 x 2160, hii ni mara nne ya saizi (pixels) ya picha inayotumiwa na mfumo wa HD kwa sasa. Inamaana yakwamba picha utakayo iona ukiwa na runinga ya 4K itakuwa safi zaidi mara nne ya ile unayoiona katika runinga ya HD, ndio sasa hebu jaribu kuvuta picha unacheza FIFA 15 na washikaji wako katika huu mzigo!

images (6)

Ulinganishi kati ya mifumo mbalimbali ya uundaji wa picha.

Kwanini mfumo huu uliitwa 4K?

Ni rahisi runinga zenye huu mfumo wa uundaji picha zilipewa jina hili la 4K kuwakilisha saizi(pixels) ya picha kwa upande wa upana. kumbuka 4K inatumia mfumo wa muundo wa picha zenye saizi (pixels) ya 4096×2160, hapa 4096 ni saizi(pixelsya upana na 2160 ni saizi (pixels) ya urefu. 4K ni jina lilotokana na ukweli kwamba upana wa picha za mfumo huu ziko katika mpangilio wa 4000(4×1000) yaani (4xK) Ingawa mfumo wa HD ama 1080p ulipewa jina hilo kutokana na saizi (pixels) ya urefu wa picha 4K Imepewa jina kutokana na saizi (pixels) ya upana wa picha

sony-4k-1

Runinga ya 4K ya SONY

http://notjusttourists.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://notjusttourists.com/about-us/articles-on-njt/ Kuna mantiki yeyote kwa kuongeza saizi (pixels) ya picha?

Ndiyo unapoongeza saizi (pixels) ya picha basi unaongeza ubora wa picha husika, picha yenye saizi (pixelsndogo basi hata ubora wake huwa mdogo kwani picha hubeba maelezo (ya kipicha ) madogo zaidi. Nieleweke kwamba ninapozungumzia kuongezeka kwa saizi(pixels) ya picha basi tunaongeza maelezo ambayo yanaambatana na ile picha, kwa maana hiyo basi maelezo yanayokuwemo katika picha inayooneshwa na  runinga ya 4K basi yatakuwa ni mara nne ya yale yanayooneshwa na runinga ya HD

SonyX90CTurntable

Mambo gani unatakiwa kuyazingatia pindi utakaponunua runinga yako ya 4K?

Moja inabidi uhakikishe upo kuanzia mita moja na nusu hadi mita nne nanusu kutoka katika runinga yako ili uweze kuona picha bora zaidi. Hili ni eneo ambalo mtu akikaa anaweza kupata picha bora zaidi.

Ili uweze kufurahia zaidi runinga yako ya 4K basi huna budi kununua kubwa kidogo maana kama utanunua runinga ndogo basi utahitajika kuisogelea karibu zaidi.

Usinunue runinga mbonyeo (curved TV) hii ni kwasababu watu watakao kuwa wanakaa pembeni hawatafaidi muonekano wa 4K

Haya sasa kazi ni kwako wewe kwenda kuitafuta hii TV Ili ujionee mwenyewe maajabu ya teknolojia!

Je una maoni, ushauri ama maswali? usisite kutuandikia katika sehemu ya maoni. Pia pitia kurasa zetu za facebook instagram na twitter 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Leave A Reply