Call Recorder ACR: Ijue app ya kurekodi mazungumzo katika simu

0
Sambaza

Simu zetu zimeyatawala maisha yetu kwa kiasi kikubwa, wengi wetu simu ndio kila kitu kwa maana michongo yote inayotuweka mjini inapita katika simu.

Kiujumla mazungumzo yetu katika simu ni muhimu sana na wakati mwingine tunahitaji kusikiliza tena mazungumzo yetu yaliyopita lakini tunayakosa, makala hii inaiangalia app ya kurekodi mazungumzo ya simu inayoitwa ACR.

App ya kurekodi mazungumzo

Je ni kosa kisheria kumrekodi mtu katika simu?

Kurekodi mazungumzo yako na mtu mwingine si kosa kisheria lakini mambo yanabadilika kutegemea na utayafanyia nini hayo mazungumzo.

Unaweza shitakiwa katika misingi ya kuingilia faragha (kuna mjadala mpana hapa na unategemea zaidi maongezi yenu yalihusu nini), kwa ujumla kama hautaki shida unaweza kumuonya mtu anayekupigia kwamba simu yake inarekodiwa (kama wanavyofanya huduma kwa wateja za mitandao ya simu).

SOMA PIA:  Arrow Launcher sasa kujulikana kwa jina la Microsoft Launcher

Unaipata wapi app hii!?

Call Recorder ACR ni moja kati ya app ambazo tumezijaribu ambayo inakupa uwezo wa kurekodi mazungumzo ya simu , app hii inapatikana katika masoko ya app kama Playstore ingawa unaweza kutumia bure lakini kuna baadhi ya mambo huwezi kufanya mpaka utakapokuwa umeilipia.

Ukiipakua app hii kabla haijaanza kufanya kazi itakutaka ukubali kabla ya kuanza kuitumia app kwamba kumrekodi mtu sio kosa kisheria. Baada ya kukubali vipengele hivyo app hii inakuwa tayari kuanza kufanya kazi, kila ukipiga simu ama kupigiwa simu itakuuliza kama unataka kurekodi hiyo simu.

SOMA PIA:  Programu wezeshi/ya kuchati ya AIM kufungwa Desemba 15

Kama unataka kila simu unayopiga ama kupigiwa irekodiwe moja kwa moja basi unaenda katika menyu > Settings > Recordings > Start recording  kisha hapa chagua Auto. Chaguo hili litafanya kila simu unayopiga ama kupigiwa itarekodiwa moja kwa moja.

app ya kurekodi mazungumzo

Utayapata wapi mafaili yaliyokwisha rekodiwa?

Simu zilizorekodiwa zote zinakaa katika ukurasa mkuu wa app hii ya ACR, unaweza kuchagua kuangalia simu ulizopigiwa tuu ama simu ulizopiga tuu ama ukaangalia orodha ya simu zote. Pia unaweza kuchuja rekodi za mazungumzo kutokana na namba za simu katika simu yako, yaani naweza kupata rekodi za mazungumzo na namba fulani tangu nianze kurekodi.

SOMA PIA:  Undani wa namba '108' kwenye app ya Siri #Maujanja

Download ACR – Google PlayStore

Je unatumia app yeyote ya kurekodi mazungumzo ya simu zako? Tuambie katika maoni ni app gani unatumia na je unaionaje!? Pia endelea kuifuatilia Teknokona katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook Twitter na Instagram.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com