Ijue Hot Knot; Sahau Kutuma Mafaili kwa Teknolojia ya Bluetooth, hii ni Bora Zaidi

0
Sambaza

Kwa wale wanaotumia zaidi simu zilizotengenezwa na makampuni ya kutoka Uchina hawatakuwa wageni na jina la Hot Knot. Hii ni huduma ya kuhamisha mafaili kutoka katika simu moja kwenda simu nyingine inayofanana na mfumo wa Bluetooth.

hotknot

Njia hii mpya inatumia screen za simu janja yako kutuma na kupokea data kutoka katika screen ya simu nyingine ambazo zimewekwa umbali wa karibu usiozidi sentimita moja.

Je njia hii inaweza kutumika kuhamisha data za aina gani?

  • Kuhamisha picha ama video.
  • kuhamisha mawasiliano kama vile namba za simu na majina katika simu.
  • Kuhamisha data za application.
  • Inaweza kuwezesha Bluetooth pairing ama kuwezesha kuunganishwa wi-fi 
  • Inaweza kutumika katika matumizi ya malipo kwa njia ya simu.
SOMA PIA:  Kufunga/kufungua 'usb ports' za kwenye kompyuta #Maujanja

Jinsi njia hii inavyofanya kazi!

Hot knot inatumia  chip za sensor za mguso kutuma taarifa za mawasiliano kwa kifaa kilichopo karibu wakati sensor za mvuto (gravity) zinatumika kuhakikisha kuna mgusano wa vifaa hivyo na kwa proximity sensor zitakuwa zinatumika kuangalia kama kuna kifaa eneo la jirani.

Hot Knot inaonekna kama ni suluhisho la gharama naafuu kutokana na ukweli kwamba teknolojia hii haitumiii kabisa transmitter na receiver.

HotKnot

Kwanini teknolojia hii inapatikana katika simu zinazotengenezwa China zaidi?

Wabunifu wa teknolojia hii ambao ni Media Tek kutoka Taiwan wanamiliki hisa katika makampuni yanayotengeneza screen za simu huko China hivyo ilikuwa rahisi kuweza kupata watengenezaji watakao ijaribu teknolojia hii huko. Hata hivyo kampuni hiyo inategemea kukua na kuufikia ulimwengu mzima.

SOMA PIA:  Ndege ya kwanza inayotumia umeme yarushwa China

Hata hivyo hii ni huduma inapatikana katika simu ambazo zimewekewa hii huduma kutoka katika kiwandani kwa maana ya kwamba huduma hii haiwezi kupatikana kwa kupakuliwa.

Kuiwezesha simu yako kutumia huduma hii (kwa simu zenye hii huduma)

  • Nenda katika mpangilio (settings) wa simu yako kisha chagua Hot Knot.
  • Simu yako itakuuliza kama unataka kuruhusu huduma hii screen ikigusana na kifaa kingine Allow data exchange when the screen touches another device? ukikubali utakuwa umeiwezesha simu kuweza kuhamisha data pale inapogusishwa na simu nyingine.
SOMA PIA:  StoreDotFlashBattery: Betri inayojaa chaji chini ya dakika moja! #Teknolojia

Makala hii iliandikwa baada ya msomaji wetu mmoja kutandikia swali facebook akitaka kujua zaidi kuhusu Hot Knot. Tuandikie nini haukielewi katika simu au kompyuta yako na sisi tutaandika makala kwa ajiri yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com