Baada ya kutoa simu ya rununu ya Honor 10, hatimaye Honor imezindua simu nyingine ya bajeti nafuu ya Honor Play 7. Simu hiyo imezinduliwa rasmi nchini Uchina.
Honor Play 7 inakuja na vipengele kadhaa vya kuvutia kikiwemo cha kamera ya mbele (Selfie) na kioo chenye kuonesha picha kwa ukubwa wa 18:9 na chenye teknolojia ya IPS LCD.
Ukubwa wa kioo wa Honor Play 7 ni inch 5.45 HD kikiwa na ung’avu wa 1440×720 pixel. Pia mfumo Endeshi ni wa Android 8.1 (Oreo).
Upande wa Prosesa ina MediaTek MT6739 Quad-core, pamoja na RAM yenye ukubwa wa 2GB na uhifadhi wa ndani (internal Storage) 16GB na unaweza kuweka Memori kadi ya ukubwa mpaka 256GB.
Honor Play 7 inakuja na kamera halisi ya nyuma yenye 13-mega pixel yenye LED flashlight. Kadhalika kamera ya mbele (Selfie) inakuja na 24-megapixel yenye LED flashlight.
Upande wa Betri ina ujazo wa 3020mAh. Upande wa mawasiliano inatumia laini mbili na zote zinasapoti 4G, ina Wi-Fi, GPS na kadhalika.
Simu hiyo inatarajiwa kuuzwa kwa Yuan 599 ambazo ni sawa na takribani shilingi 210,000 za kitanzania.