Imeripotiwa Kuwa Kampuni Ya Apple Ipo Katika Mchakato Wa Kurudisha Kiwanda Chake Marekani!

0
Sambaza

Kampuni nguli katika maswala ya teknolojia ambayo ina jina kubwa kupitia uzalishaji na uuzaji wa simu zake za iPhone imeripotiwa kuwa inafanya mchakato ili kuangalia uwezekano wa kampuni hiyo kurudi na kufanya uzalishaji wake Marekani.

Ripoti zinasema kwamba kampuni hiyo ya Apple imekuwa ikiwauliza washirika wake kuanza kufanya uchunguzi juu ya kuanza kufanya uzalishaji wake huko Marekani.

Kutoka katika chanzo cha habari (Gazeti) cha nchini japan Nikkei, kimeripoti kuwa Apple imewasogelea Foxconn na Pegatron (ambao hawafanyi vizuri kama inavyotarajiwa) ambao pia wanahusika kwa kiasi kikubwa katika uunganishaji wa vifaa mbali mbali katika simu za iPhone

SOMA PIA:  WhatsApp yaleta status zenye mtindo wa Snapchat, Facebook waendelea kuiba vizuri!

191964_white-apple-inc-mac-pc-iphone-ipad-2560x1600-wallpaper_wallpaperbeautiful_86
Foxconn ni kwamba iko tayari kuangalia uwezekano lakini kampuni ya Pegatron yenyewe bado inasua sua na pia inatolea macho sana sehemu nzima ya gharama.

Wengi wanasema kuwa pengine hili limetokea baada ya raisi mpya wa marekani bwana Donald Trump kusisitizia katika kampeni zake kuwa makampuni ambayo yanazalisha bidhaa na yapo marekani basi hayana budi kufanya shughuli zote za uzalishaji palepale marekani.

Trump vile vile alisikika na kuonekana akiitaja kampuni ya Apple wazi wazi juu ya swala hili. Bwana Trump alisema kuwa “Tutaifanya Apple Kuanza Kutengeneza Kompyuta Zao Na Vitu Vingine Katika Nchi Hii, Kuliko Nchi Zingine”.

SOMA PIA:  StoreDotFlashBattery: Betri inayojaa chaji chini ya dakika moja! #Teknolojia

Pengeni labda usemi huo unaweza ukawa umechochea hili kwa namna Fulani lakini hata hivyo maneno haya yalisemwa na Bwana Trump mwaka 2016 mwezi wa Kwanza na Apple imeanzisha mchakato mzima wa uchunguzi ndani ya mwezi wa 6 mwaka huu.

apple-building

Moja Katika Ya Majengo Yanayomilikiwa Na Apple

Kwa jicho langu ni kwamba kampuni ya Apple kama ikiamua kufanya hivi itakuwa haipati faida kama ile ambayo ilikua inaipata mwanzo. Kumbuka Apple bado inafanya uzalishaji wa simu hizi huko nchini china ambapo kuna nguvu kazi ya gharama rahisi kabisa tofauti na ikienda kufanya uzalishaji wote kule.

SOMA PIA:  Tetesi: Gharama ya iPhone 8 kuwa zaidi ya sh. 2.2M

Licha ya nguvu kazi ya gharama kuna mambo mengine mengi ambayo yataifanya kampuuni hiyo kupata faida ndogo, ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment ni nini mtazamo wako.

Temebelea TeknoKona kila siku, kumbuka kuwa TeknoKona ndio mtandoa wako nguli kwani kila siku tunakuletea habari na maujanja kadha wa kadha ambazo zinahuzu swala zima la Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com