Hivi ushawahi piga picha nzuri, ukaipeleka katika mtandao wa Instagram ukaiitilia mbwembwe kibao na ikatoka poa. Lakini ukakumbuka kuwa sio muda mzuri wa kuipost?
Yaani ukiipost kwa muda huo labda unaweza usipate like nyingi kama ungeituma kwa muda mwingine? Nadhani hiyo imeshatutokea sana tuu.
Sasa kabla hujaamua kutoka katika mtandao huo (bila ya kupost picha/video hiyo) na kupoteza taarifa zako, mtandao wa instagram unaripotiwa kuwa katika uandaaji wa kipengele cha ‘Save As Draft’.
Kwa kutumia kipengele hichi jambo la kutoka katika mtandao na kupoteza taarifa zako kisa hujaposti kwa muda husika halitakuwepo tena. Hapa utaweza kuhifadhi kazi yako (picha/video) na kisha utaweza kuituma baadae katika mtandao huo.
Kwa sasa zoezi hili zima lipo katika majaribio lakini kwa watumiaji baadhi (ambao wamechaguliwa) ndio wanatumia huduma hii kwa sasa. Kama kawaida na sisi ambao bado haijatufikia hatuna budi kuisubiria kwa hamu.
Huduma hii itakuwa inapatikana baada ya mtu kuchagua kurudi nyuma wakati akiwa anatengeneza picha yake. Hapo mtandao wa Instagram Utakuuliza kama unataka kuhifadhi kazi hiyo (Save As Draft).
Kwa Kutumia Mtandao Wa Twitter Watu Mbalimbali Wamekuwa Wakiisifia Huduma Hii
Here's a look at @instagram's "Save Draft" functionality, currently being tested amongst a subset of users pic.twitter.com/dfgOw9Bdhj
— Patrick (@Plambey) August 10, 2016
https://twitter.com/BrookeALarson/status/761648006588424192
Ili kuweza kutumia huduma hii itakavyotoka kwa watu wote, itakubidi uwe na Instagram ya toleo jipya zaidi. Tuisubirie basi