Inasemekana Twitter Inatafuta Mnunuzi Wa Vine! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Inasemekana Twitter Inatafuta Mnunuzi Wa Vine!

0
Sambaza

Twitter bado haijakata matumaina kabisa kama tulivyokuwa tunazani. Kwa sasa wameona bora kupitia tena ofa walizoletewa na watu ambao wanataka kununua mtandao wa Vine

click

buy celebrex cheap Ofa hizo kama zitakuwa na faida kwao basi itakuwa ni jambo la busara kuuza mtandao huo kuliko kuacha kuendelea kuutumia.

see url Taarifa zilizotoka ni kwamba kampuni la Twitter limepata ofa nyingi sana za makampuni mengine kutaka kununua mtandao huo wa Vine, ofa hizo nyingi zilitoka katika makampuni mengi kutoka bara la Asia.

Mtandao wa kijamii wa Vine unamilikiwa na Twitter.

Mtandao wa kijamii wa Vine unamilikiwa na Twitter.

Japokua hakuna ushaidi wa moja kwa moja lakini inasemekana moja kati ya makampuni ambayo yalionyesha nia hiyo ni pamoja na kampuni ya Line, ambayo inajihusisha na mambo ya magemu na meseji huko nchini Japan.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Kupiga simu kwa njia ya sauti/video kwenye makundi inawezekana

SOMA PIA: Kifo Cha Mtandao Wa Vine Ndio Hiki!

App Ya Vine

App Ya VineVine

La kushangaza ni kwamba japokuwa makampuni mengi yameonyesha nia lakini hakuna kampuni hata moja ambalo limetoa ofa ambayo inazidi dola milioni kumi za kimarekani. Kumbuka Twitter ilisema itaachana kabisa na mtandao huo bila hata ya kufikiria kuuza.

Pengine hilo ndio jambo ambalo limewafanya watu watake kuununua japokuwa hata kwa kiasi kidogo. Lakini swali bado linabaki pale pale, je kampuni itakubali ofa hizo (licha ya kuwa ni ndogo sana).

mnunuzi wa vine

Logo Ya Vine: Je mnunuzi wa vine atapatikana?

Kwa mtazamo mwingine ni kwamba bado kampuni la Twitter linaweza likapata faida endapo litapata mnunuzi mzuri wa mtandao wa Vine ambaye atauendeleza na kisha Twitter itakua inafaidia pale mtu anapo’share’ kitu chake katika mtandao wa Twitter (yaani ule muingiliano wa Vine na Twitter).

INAYOHUSIANA  Fahamu Mambo Mapya Yanayokuja Kutoka WhatsApp

Ningependa kusikia kutoka kwako, je wewe unahisi Twitter itauza kweli mtandao wake wa vine au mtandao utakufa tuu kama kawaida inavyodhaniwa? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka kutembelea TeknoKona kila siku kwa habari na maujanja mbalimbali yanayohusu teknolojia.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.