India wapiga hatua nyingine katika sayansi ya Anga! #Teknolojia

1
Sambaza

India imeendelea kupigana vikumbo na mataifa yaliyoendelea katika mbio za utafiti juu ya sayansi ya anga baada ya kufanikiwa kufanya majaribio ya space shuttle ambayo inaweza kutumika zaidi ya mara moja.

Nchi kama Marekani Japan Urusi na mataifa mengine ya ulaya yamekwisha pata teknolojia hii mengi yameanza kutumia hivi vifaa karibuni.

Jumatatu iliyopita wakala wa mambo ya anga wa India ilitangaza kwamba majaribio ya Space shuttle yamefanyika kwa mafanikio na hivyo teknolojia iliyotumika kutengeneza kifaa hicho cha mfano imeonekana kuwa inafaa kutumika.

India

space shuttle hiyo ikiwa katika moja ya hatua za majaribio

Kulielewa tukio hili basi inabidi tuigawanye teknolojia ya anga katika makundi mawili, teknolojia ya kurusha vifaa kama space shuttle ama satellite na pia teknolojia ya kurusha roketi ambazo hubeba satellite na Space shuttle. Teknolojia zote mbili zinachangamoto nyingi moja wapo ni gharama kuwa kubwa kutokana na ukweli kwamba teknolojia hizo mbili kwa muda mrefu zimekuwa na uwezo wa kutumika mara moja tuu kitu ambacho kilifanya gharama za uendeshaji kuwa juu sana.

SOMA PIA:  Namna ya kuhamishia App katika Memori kadi! #Maujanja

Teknolojia ya vifaa vinavyorushwa katika anga tayari imekwisha fanyiwa utafiti kwa kiasi kikubwa na hivi sasa zipo nchi ambazo space shuttle pamoja na satellite zinaweza kutumika katika safari zaidi ya moja, ila kwa nchi za Asia India imekuwa ya kwanza kufanya majaribio haya.

India ilipeleka space shuttle yenye urefu wa futi 22 kwenda katika umbali wa kilometa 65 kutoka usawa wa bahari na kisha kukirudisha chombo hicho duniani. Hii inamaana kwamba India sasa inayoteknolojia ya kupeleka space shuttle kwenda angani kisha kurudisha duniani tayari kwaajiri ya kuitumia tena.

India wapiga hatua

Mchoro kuonesha muonekano wa Space shuttle hiyo iliyorushwa.

India ni moja ya nchi zinazoendelea ambayo inawekeza kiasi kibubwa katika utafiti wa anga, Ingawa bado ni safari ndefu mpaka kufikia hatua ya kuweza kutengeneza space shuttle ambayo itawezakupeleka wanasayansi angani na kisha kuwarudisha duniani lakini hii ni hatua muhimu sana katika sayansi ya Anga.

SOMA PIA:  Huawei Wazalisha Simu Chache Zenye Chata La KFC Huko China!

India inaonesha njia sahihi ambayo mataifa yanayoendelea hasa ya Afrika mashariki yanaweza kuchukua katika sayansi badala ya kuendelea kuwa watazamaji na watumiaji wa teknolojia zinazobuniwa na mataifa yaliyo endelea.

Makala hii imeandikwa kwa msaada kutoka kwa mitandao ya habari ambayo ililipoti tukio hili kama vile Aljazeera.

Soma: Space X yafanikiwa kutua roketi katika meli

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.
error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com