India kupitia shirika lake mambo ya anga limefanikiwa kurusha setelaiti 20 angani, hii ni namba kubwa zaidi ya setelaiti kurushwa na shirika hilo na pia gharama za misheni hii ni ndogo zaidi ukiringanisha na misheni kama hizi zilizofanyika katika mataifa mengine.
India imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya ushawishi katika mambo ya anga baada ya shirika la nchi hiyo la mambo ya anga kupeleka setelaiti 20 kwa mkupuo angani leo. Tukio hili linaiweka India nafasi ya tatu nyuma ya Russia na Marekani ambao walikwisha peleka Setelaiti nyingi zaidi.
Nyingi ya setelaiti hizo ishirini zinatoka kwa wateja kutoka Kanada Ujerumani Indonesia na Marekani, India sasa inakuwa nyuma ya Rusia ambao waliweza kurusha setelaiti 33 hapo mwaka 2014 na pia nyuma ya Marekani ambao kupitia NASA waliweza kurusha setelaiti 29 mwaka 2013.
Pamoja na yote mzigo huo unahusisha pia setelaiti mbili ambazo zimetengenezwa na vyuo viwili kutoka nchini humo.
Mtandao wa Aljazeera umeripoti kwamba Waziri mkuu wa nchi hiyo ambaye siku zote amekuwa ni mtu ambaye anaungamkono jitihada hizo amesema kwamba haya ni mafanikio makubwa kwa taifa hilo la barani Asia na akawapongeza wanasayansi walioweza kufanikisha hilo.
Mwaka 2008 India iliweka rekodi kwa kuwa ndiyo taifa la kwanza kurusha setelaiti 10 kwa wakati mmoja rekodi ambayo ilikuja kuvunjwa na Marekani kisha baadae Urusi. India ina kuwa kimbilio la makampuni ambayo yanataka kurusha setelati angani kwa gharama naafuu, biashara ya kurusha satelaiti angani inazidi kukua na nchi mbali mbali zimekuwa zikijaribu kufanya biashara hii.
Soma Zaidi: India wapiga hatua nyingine katika sayansi ya anga
Endelea kufuatilia Teknokona kwa habari motomoto za teknolojia katika lugha yako adhimu.
One Comment
Comments are closed.