InstaAgent : App Iliyokua Inaiba Password za Instagram Yashtukiwa

1
Sambaza

Apple na Google wameondoa app ya InstaAgent iliyokuwa inakuja kwa kasi katika masoko yao ya apps kufuatia shutuma za kwamba app hiyo huiba nywila (password) na data za watumiaji wake.

App ya InstaAgent ilikuwa ni moja ya apps zinazoshushwa zaidi katika masoko ya apps ya Google na Apple. Google na Apple wameiondoa app hiyo baada ya mmoja wa watengenezaji kuonesha ushahidi kuwa InstaAgent wanachukua nywila na kuzihifadhi sehemu isiyojulikana.

Picha ikionesha kuwa kitumizi hiki kilikuwa kinaongoza katika vitumizi vya bure vya Apple store

Kitumizi hiki kinafanyeje kazi?

Kwa mujibu wa mtengenezaji huyo wa apps aliyegundua tatizo hilo ni kwamba InstaAgent ( ambayo katika inajulikana kama “Who Viewed your Profile-InstaAgent ) ikishushwa na kuwa installed kwenye simu huweza kuchukua nywila na jina la mtumiaji wa Instagram baada ya hapo app hiyo huweza kuingia katika akaunti yako na ku post picha na mambo mengine bila ruhusa yako.

SOMA PIA:  Jinsi ya kuzuia iOS 11 kumaliza chaji ya simu yako ndani muda mchache

Je ufanye nini kama ulikwisha tumia app hiyo?

Kama na wewe ulitokea kuishusha app hii basi upo katika orodha ya waasilika wa tatizo hili na Instagram wametoa suluhisho la jambo hili ambalo kwanza ni kuiondoa app hii kama bado unayo, na pili ni kubadili nywila(password) yako haraka iwezekanavyo.

airtel tanzania bando

Kuwa makini sana na apps unazopakua kwenye simu yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

1 Comment

  1. Pingback: InstaAgent : App Iliyokua Inaiba Password za Instagram Yashtukiwa | Teknolojia

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com