Instagram Inaifanyia Majaribio InstaLive Kwenda Katika 'Screen' Inayogawanyika! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Instagram Inaifanyia Majaribio InstaLive Kwenda Katika ‘Screen’ Inayogawanyika!

0
Sambaza

Wengi wanapenda kwenda Live katika mtandao wa kijamii wa Instagram. Mtandao huo umekua ni moja ya sehemu maarufu ya kurusha matokeo ya moja kwa moja kwa nddugu, jamaa na marafiki.

http://princetonforrestalcenter.com/

http://cfch.net/calendar/action~month/exact_date~1533873600/request_format~html/ Kwa sasa Mtandao huo uko katika majaribio ya kuangalia kama zoezi hilo litafanikiwa huku screen ikiwa inagawanyika.

see Instagram

Yaani hapa iko hivi wakati mtu anawekwenda Live katika mtandao huo ana uwezo wa kumualika mtu mwingine nae akaenda Live.. Kitakachofanyika ni kwamba ‘Screen’ itagawanyika mara mbili na kisha zitaonekana video mbili (Live).

Mtazamaji atakuwa na uwezo wa kuziona video zote hizo mbili na pia atakuwa na uwezo wa ku’comment katika video hizo kama kawaida.

Hivi Ndivyo ‘Screen’ Itakavyoweza Kujigawa Katika Video Mbili Za Live

Mpaka sasa haijulikani siku kamili ambapo kipengele hichi kitaachiwa rasmi, kwani kwa sasa kampuni imechagua watu wachache tuu kukifanyia majaribio.

INAYOHUSIANA  Intagram yaenda mbali, sasa inawatumiaji hai bilioni moja

Kampuni imesema dunia nzima itegemee kipengele hichi katika miezi ya usoni.

Kampuni kwa sasa inafanya vizuri sana kwani inaufanya mtandao usionekane kama ni wa ku’share picha tuu, bali unaonekana una mambo mengi kama vile storie, LiveStream na mambo mengine mengi.

Mtandao unazidi kupiga hatua kila siku na kama kipengele hiki kikitoka duniani kote basi itakua ni msaada mkubwa sana kwa watu. Hebu fikiria msanii mmoja anaweza akaenda Live na msanii mwenzake katika ukurasa mmoja.

Ningependa kusikia kutoka kwako, wewe hii umeipokeaje? je una neno gani la kiuwaambia Instagram? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!,

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.