Instagram kuja na app kwa ajili ya kuchati tu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Instagram kuja na app kwa ajili ya kuchati tu

0
Sambaza

Umuhimu wa kuwa na app ya kufanya mazungumzo kwa njia ya maandishi  umeonekana na app hiyo imeelezwa ipo katika hatua ya majaribio katika baadhi ya nchi.

see url

source site Direct ndio jina la app hiyo mpya ambayo ipo katika hatua ya majaribio ambayo inalenga zaidi kuongeza faragha na uhuru zaidi wa kufanya mawasiliano kwa marafiki kutumiana ujumbe wa maandishi kama ilivyo kwenye Facebook Messenger pamoja na WhatsApp ambazo zote kampuni mama ni Facebook.

Kama ulikuwa ufahamu………..

Mwaka 2012 Facebook ilinunua Instagram kwa karibu $1 bilioni na kufanya kufikia idadi ya makapuni pacha kuwa matatu; WhatsApp, Instagram na Facebook Messenger yenyewe.

Facebook imeonekana ikitaka kuwavutia watu wazidi kutumia mitandao ya kijamii na hata ikionekana kuwalenga watoto wenye umri mdogo kwa kuleta go site app mahususi kwa ajili ya watoto wa umri huo (miaka 13 kurudi chini), pamoja na mambo mengine mengi kwenye programu tumishi nyingine inazozimiliki.

INAYOHUSIANA  Instagram Lite Sasa Yaanza Kupatikana.

Upatikanaji wa app ya Direct.

App hii bado haipatikani kwa nchi nyingi tu ila katika baadhi ya nchi Chile, Israeli, Itali, Ureno, Uturuki na Uruguay zikipatikana kote kwenye Android na iOS. Haijafamika kabisa iwapo app hiyo itaanza kupatikana mwaka huu kwingineko duniani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinaamini app hiyo itaanza kupatikana mwakani.

Baada ya kupakua app ya Direct moja kwa moja kipengele cha “Direct Message” kwenye app ya Instagram hakitakuwepo na badala yake sasa mtu ataweza kutumia app ya Direct kwa ajili ya kuchati.

App ya Direct: Ukishaanza tu kutumia app hii marafiki zako wote kwenye Instagram utawaona kwenye na utaanza kuwasiliana nao huko kwenye app ya Direct.

 Kwenye hii app ya Direct mtu atakuwakupiga picha na kuweza kuiwekea nakshi nakshi kama vile filters na mambo mengine pamoja na kuweza kuituma muda huo huo kwenda kwa rafiki yake. Je, unadhani hii itawavutia watu kuongeza idadi ya wanaotumia Instagram?

Vyanzo: Techrunch, The verge, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.