fbpx

Instagram Lite Sasa Yaanza Kupatikana.

1
Sambaza

Baada ya kufikia watumiaji hai Bilioni moja, sasa Instagram imeonesha wazi kuwa inataka kuendelea kupata watumiaji wengi zaidi pengine kuwa mojawapo ya mtandao unaongoza kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani.

http://sociallighters.com/uptimebot org.php

Siku ya jumatano Instagram imeachia toleo jepesi (Lite) ambalo limeanza kupatikana kwa watumiaji wa Android.

Instagram imeamua kuachia toleo hilo jepesi ikiwa ni maalumu kwa nchi zinazoendelea na watu wengine duniani ambao wanatumia simu ambazo zina nafasi ndogo pamoja na maeneo ambayo kuna matatizo ya mtandao.

Ukiwa na toleo jepesi (Lite)  la Instagram utaweza kufanya mambo yote kama mtumiaji wa kawaida mwenye programu tumishi halisi.

Mambo ambayo hautaweza kufanya kwa sasa ni kupakia video pamoja na kusambaza ujumbe  (message) kwa njia ya kushirikisha moja kwa moja kwa marafiki jambo ambalo uongozi wa Instagram umeeleza upo kulifanyia kazi zaidi.

Instagram Lite inategemea kuongeza zaidi watumiaji wa Instagram hasa kutoka nchi zinazoendelea kama Tanzania.

Instagram Lite itawawezesha watumiaji kuweza kufurahia namna rahisi zaidi ya kupakia picha huku nafasi katika simu zao ikiwa ya kutosha na hivyo kuleta urahisi zaidi wakati wa utumiaji.

Kutokana na toleo hilo, kuna uwezekano mkubwa wa ongezeko la watumiaji hasa kutoka nchi zinazoendelea ambazo zimekua zikikumbwa na matatizo ya kimitandao pia na uwepo wa vifaa duni ambapo kwa toleo hili itakua rafiki kwao.

Kwa sasa imeanza kupatikana nchini Mexico, lakini siku zijazo itaanza kupatikana duniani kote.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mwandishi Pia mpenzi mkubwa wa masuala ya Teknolojia, Napenda Kujifunza, Karibu Tujifunze Pamoja.