Watumiaji na wapenzi wa mtandao wa kijamii wa Instagram kaeni mkao wa kula kwani baada ya muda kidogo mambo yatakuwa ni bombaa!.
Hivi karibuni watu ambao unaowafollow au hata wale wanao kufollow nyote mtakuwa na uwezo wa kujua mtu anaanisha kitu gani kulingana na lugha ambayo ameitumia
Mtandao huo wa Instagram utawezesha hilo kwani imeleta kipengele chake kipya kinachohusisha utafsiri wa lugha
Hii imekuja baada ya pale watu walipokuwa wana share mambo mengi ya moyoni kwa kutumia picha tuu kwani wengi walikuwa wanashindwa soma ujumbe ambao ulikua umeambatana na picha hizo (lugha Gongana!)
Huduma hii itaanza kutumika rasmi mwezi ujao na lakini haitaishia katika kutafsiri ujumbe ule ulioambatana na picha tuu bali hata katika maeneo kama ya BIO na kadhalika.
Lengo kubwa la Instagram kufanya hivyo ni kuwaleta wanajamii karibu kabisa kwa kuhakikisha kuwa wanatokomeza kabisa hali ya kushindwa kuwasiliana kutokana na vizingiti kama vile lugha
Mpaka sasa huduma hiyo inajumuisha lugha 24 tuu ambazo zipo katika mfumo mzima. Hii haitaishia hapa kwa Instagram wapo katika mchakato mzima wa kuongeza namba hii
Utaweza kupata utafsiri wa lugha Fulani mtu aliyoandika katika ukurasa wake wa Instagram kama lugha hiyo ipo miongoni mwa zile ambazo zimechaguliwa kuweza kupatiwa utafsiri. Kama haipo basi huna budi kuipeleka katika lugha nyingine ambayo unaweza kuitafsiri kwa urahisi
SOMA PIA : Instagram yafikisha watumiaji Nusu Bilioni