Kwa kiasi kikubwa Facebook wanazidi kudhihirisha ya kwamba kushindwa kwao kuinunua Snapchat kuna maanisha watahakikisha wanaiba kila sifa nzuri ya app hiyo na kuiweka kwenye Instagram.
Kuanzia sasa app ya Instagram itakupa taarifa pale mtu unayechati naye kupitia eneo la Instagram Direct ataamua ku’screenshot mazungumzo yenu.
Tayari hivi karibuni tuu Instagram walileta uwezo wa mazungumzo (messages) yanayopotea yenyewe baada ya kusomwa, sifa ya muda mrefu kwa watumiaji wa Snapchat.
Kumbuka utapewa taarifa juu ya mtu ku’screenshot mazungumzo ya Instagram Direct tuu, tena yale ambayo umechagua kufutika baada ya mwingine kupokea na kusoma ujumbe.
Hii haitahusisha picha unazoweka kwenye akaunti yako kikawaida – Timeline.
Hakikisha unasasisha (update) app yako ili kuweza kupata toleo la kisasa zaidi. Kingine kipya katika Instagram ni pamoja na uwezo wa kutuma video za LIVE.