Instagram: Wafanya Maboresho Zaidi, Furahia 'Groups' n.k - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Instagram: Wafanya Maboresho Zaidi, Furahia ‘Groups’ n.k

0
Sambaza

Vita katika apps za kuchati zinazidi kupamba moto. Instagram nayo yaleta mambo mapya yanayozidi kuifanya ishindane moja kwa moja na apps zingine kama vile Snapchat. Kila apps iliyo kwenye simu janja zetu inataka tutumie muda mwingi zaidi kwake kuliko kwenye apps zingine.

Snapchat ni app ya kuchati ya iOS na Android ambayo inakua kwa kasi sana kwa sasa. Inawatumiaji zaidi ya milioni 100 na sifa zake kubwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa mtu mmoja mmoja kutumiana picha zenye maneno n.k na ujumbe huo kufutika baada ya muda mfupi wa kusomwa.

Instagram kupitia sasisho (update) mpya wameleta mambo mapya katika app yao ya takribani watumiaji milioni 300.

INAYOHUSIANA  Fahamu Mambo Mapya Yanayokuja Kutoka WhatsApp

Mwanzo unapoweka kitu Instagram kilikuwa kinaonekana kwa watu wote wanaokufuatilia katika huduma hiyo, kuanzia sasa utaweza kuweka picha na kuwaonesha watu kadhaa tuu badala ya wote wote. Mazungumzo yenu yote mtakayofanya chini ya picha au video hiyo ni nyie tuu ndio mtaweza kuyaona.

Uwezo wa kuchati kwa kutumia picha na maneno kati ya watu wawili au ktk kundi

http://bennettracingengines.com/348r.html Uwezo wa kuchati kwa kutumia picha na maneno kati ya watu wawili au ktk kundi

Instagram wanaamini kufanya hivi kutawawezesha watumiaji wao wengi kutumia muda mwingi zaidi ndani ya app yao na kupunguza kufanya mazungumzo mengine ya namna hiyo kwenye apps nyingine kama vile Snapchat.

Uwezo wa kutuma picha kwa watu au kundi flani tuu

Uwezo wa kutuma picha kwa watu au kundi flani tuu

Inasemekana kwa sasa vijana wengi wanapendelea kufanya mazungumzo mengi kupitia njia za kutumiana picha katika apps kama vile WhatsApp, Instagram na Snapchat. Kwa uamuzi huu Instagram wanatemea kuweza kuwavutia watu wengi zaidi ambao vinginevyo wangekuwa wanafanya mazungumzo yao katika apps kama Snapchat.

INAYOHUSIANA  Kifaa cha kupima malaria bila ya damu chaundwa nchini Uganda

Je una maoni gani na mpya hii? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja Tanzania kwa habari na maujanja ya kiteknolojia.

Bofya Kupakua;

 [socialpoll id=”2292414″]

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply