Instagram yafikisha watumiaji Nusu Bilioni

2
Sambaza

App maarufu ya mambo ya picha na video – Instagram yafikisha watumiaji milioni 500, hii ni idadi ya watumiaji milioni 100 zaidi ukilinganisha na mwezi wa 9 mwaka jana.

instagram yafikisha watumiaji

Mtandao wa kijamii huu unaomilikiwa na Facebook umetoa taarifa rasmi ya idadi ya watumiaji wake masaa machache yaliyopita.

Katika taarifa hiyo pia wameonesha idadi ya watumiaji hai kwa siku kuwa ni watumiaji milioni 300, yaani hii inamaanisha kuna watumiaji milioni 300 wanaofungua app ya Instagram kila siku.

Today, we’re excited to announce our community has grown to more than 500 million Instagrammers — more than 300 million of whom use Instagram every single day. Our community also continues to become even more global, with more than 80 percent living outside of the United States. As you’ve captured and shared the moments happening around you, you’ve formed incredibly varied and diverse communities. Whether you’re an illustrator, a sneakerhead or an astronaut on the International Space Station, every photo and video you share helps bring people closer to friends and interests, broaden perspectives and inspire a sense of wonder. You’ve made Instagram a place where the everyday and the epic are always within reach. Thank you for your creativity, your openness and your passion for sharing your worlds with one another. We can’t wait to see what you create next.

A video posted by Instagram (@instagram) on

Pia wanajivunia kuona ukuaji wa watumiaji wa app hiyo unakizidi kuongezeka nje ya nchini Marekani, katika taarifa yao wamesema zaidi ya watumiaji asimilia 80 ya app hiyo wapo nje ya nchini Marekani.

SOMA PIA:  AppStore: Apple yaondoa VPN kwa simu za iPhone nchini China

Idadi ya watumiaji wa mtandao huu wa kijamii umekua mara mbili ndani ya miaka miwili, kampuni ya Instagram na app yake ilinunuliwa mwaka 2012 na mtandao mkubwa wa kijamii wa Facebook kwa takribani dola bilioni 1 za Kimarekani.

Je wewe ni mtumiaji wa kila siku wa app ya Instagram? Hongera, ni mmoja kati ya watu milioni 500 duniani kote!

Chanzo: Instagram Blog

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com