Baada ya kuiga Stories kutoka Snapchat Instagram imeendelea kuiga mitindo ya Snapchat baada ya kutambulisha chaneli kwaajiri ya video za matamasha mbalimbali katika kipengele cha Discover.
Mtindo huu wa Chaneli kwaajiri ya matukio ya kwenye matamasha imeanza kupatikana kwa watumiaji walio Marekani inakuwa na mchanganyiko wa video mbalimbali kutoka katika tamasha fulani.
Niwazi kwamba Facebook na Instagram wanawekeza kwa kiasi kikubwa katika video, tayari Instagram wamekwisha leta kipengele cha video ambazo mtumiaji anaweza kupenda kuzitizama ambapo Instagram kutokana na marafiki wako na vitu unavyoangalia wanakuletea video ambazo wanadhani kwamba utazipenda kuzitizama.
Chaneli mahususi za matukio fulani zimekuwepo katika app ya Snapchat kwa muda sasa na pengine kwa kiasi fulani zimechangia mafanikio ya mtandao wa Snapchat ambao hauna muda mrefu katika soko. Instagram na mitandao mingine imekuwa ikijaribu kupata watumiaji hai wengi zaidi kila siku kwa kuiga yale ambayo Snapchat imefanya katika kujipatia watumiaji wengi.
Instagram inaonekana kubadili muelekeo na kujikita pia katika video, hii ni kutokana na ukweli kwamba watumiaji wengi katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakisambaza na kuangalia video zaidi. Instagram imekwisha ongeza urefu wa video ambazo watumiaji wanaweza kutuma katika app hiyo jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa idadi ya video zinazotumwa.
Ingawa kwa Tanzania na nchi za Afrika mashariki bado chaneli hii ya video kutoka katika matukio fulani bado haijaja lakini pindi itakapo fika basi mtandao wa Teknokona utakujulisha ili uweze kuijaribu na kutupatia mrejesho wako.
Habari hii iliripotiwa na mtandao wa RECODE