Instagram yaleta uwezo wa kufuatilia Hashtag

0
Sambaza

Instagram imekuwa katika umaarufu kwa kila kitu kipya ambacho mtandao huo wa kijamii unaboresha kwenye app yake na kufanya kuzidi kuwavutia watu wengi tu ulimwenguni.

Utumiaji Hashtag (#) au kwa tafsiri ramsi alama ya reli umekuwa maarufu sana katika mtandao wa Twitter na bado ni maarufu ikitumika kufikisha ujumbe fulani kupitia mtandao wa Twitter na hata kwenye mitandao mingine ya kijamii. Kujua zaidi kuhusu Hashtag BOFYA HAPA.

Lengo la kuleta Hashtag kwenye Instagram.

Hapo awali ili kuweza kupata stori/chapisho fulani ilibidi uingie kwenye sehemu ya kutafuta na uaindike ukurasa au jina la mtu Instagram kuweza kuona machapisho yake. Hashtag kwenye Instagram imekusanya machapisho/stori maarufu na kuweza kufuatilia na kuzipata kwa urahisi kabisa, mathalani #TeknoKona.

MAtumizi ya Hashtag kwenye Instagram: Hashtag inafanya machapisho ya mhusika kuweza kuonakna mara kwa mara na kufanya machapisho hayo kuwa maarufu.

Katika kuepuka mkanganyiko wa stori/machapisho kwenye Instagram, mtu anaweza kutafuta akaunti/ukurasa ambao hautumii alama ya reli (#) mwanzo wa kichwa cha habari cha chapisho vilevile inawezekana kutafuta chapisho chapisho/akaunti ya mtu inayoanzia na Hashtag.

Utumiaji wa Hashtag kwenye Instagram utawezesha chapisho/akaunti husika kuwa katika uso wa mbele mara kwa mara kwa wale wanamfuata kutokana na Intagram kuyaleta mbele machapisho hayo mara kwa mara.

Ni vyema kwa watu wenye akaunti za kibiashara kwenye Instagram wakaanza kutumia alama ya reli (#) kwenye kurasa zao ili kuwezesha kile wanachokitangaza kuweza kuonekana mara kwa mara na hivyo kupata soko kwa haraka zaidi.

Vyanzo: The Independent, Techrunch, Gadgets 360

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  WhatsApp Business yaanza kupatikana; Sasa unaweza ukafungua akaunti ya kibiashara
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com