fbpx

Instagram yazidi kuiga Snapchat

0
Sambaza

Instagram wameweka wazi ya kwamba wameiga mfumo wa Snapchat kuwaruhusu watumiaji kurekodi picha ama video ambazo zitakaa kwa muda usiozidi masaa 24.

can you buy Lyrica at walmart

Instagram inategemewa kuanza kusambaza masasisho ambayo yataleta uwezo wa kuweka stori (za picha ama video) ambazo zitadumu kwa masaa ishirini na nne na kupotea kitu ambacho wamekubali kuiga kutoka Snapchat.

Instagram kuiga snapchat

Kwa hali ilivyo sasa watumiaji wengi hujikuta inawabidi kuweka katika Instagram picha zile tu ambazo zimetoka vizuri ama wamtetokelezea lakini ukweli nikwamba zipo picha nyingi sana tunapiga kila siku, Instagram wanataka kuwa zaidi ya mtandao ambao tunaweka picha zile tu tulizotokelezea wanataka iwe ni mahali ambapo tunaweka hata video za kizushi kama za kutabasamu katika pozi tofauti.

Instagram imeamua kuleta huduma ambazo zilikuwa zinawafanya watu waende kutumia Snapchat, katika masasisho yanayokuja ya Instagram kutakuwa na kipengere cha Stories ambacho kimsingi kimeigwa kutoka Snapchat.

INAYOHUSIANA  Tanesco kuja na makundi kwenye WhatsApp

Watumiaji wa instagram wataweza kuweka picha kwa njia ya kawaida ambazo zitadumu katika akaunti zao kwa muda mrefu ama wanaweza kuweka kama stories ambazo zitadumu kwa masaa 24 kisha kupotea kama vile ilivyo kwa Snapchat.

instagram kuiga

Muonekano wa Stories katika instagram

Hatua hii imepingwa na baadhi ya watumiaji wahafidhina ambao wanaona kuiga Snapchat ni jambo baya, Instagram wao wanaamini kwamba maisha yamebadilika na kwa sasa ni wazi kwamba ili waweze kushindana na Snapchat moja ya si ni kuiga mazuri ya mtandao huu mpya.

Je unasemaje juu ya habari hii ya Instagram kuiga ujanja wa Snapchat? tuambie katika maoni

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.