Instagram yazidi kuwabana wenye matusi

0
Sambaza

Instagram inaangalia uwezekano wa kupunguza matusi na maneno ya chuki katika mtandao huo.

Wanafikiria kuleta kwa watumiaji;

  • uwezo wa kuchuja maoni ambayo wafuasi wa mtumiaji wanaweza kuandika
  • uwezo kwa watumiaji kuzuia maoni kabisa katika picha zao.

Kwa hapa bongo katika mitandao Instagram ndio mtandao unaoongoza kwa watu kutukana, kumekuwa na makundi ambayo yamekuwa yakirushiana matusi mazito.

instagram-keyboard-app-take- matusi

Kwa mujibu wa jarida la Washington Post ni kwamba sasisho hili litaleta uwezo kwa watumiaji wa Instagram kuweza kuchuja maoni kwa kusema baadhi ya maneno ambayo hawataki maoni yawenayo, kwa mfano mtumiaji anaweza kutaja matusi yote ambayo iwapo mfuasi wako atataja basi maoni yake hayatachapishwa katika picha yako.

SOMA PIA:  WhatsApp kurahisisha mawasiliano baina ya watu na makampuni/biashara

Masasisho haya pia yataweza kuwaruhusu watumiaji wa mtandao wa Instagram kuweza kuzuia kabisa maoni kutoka kwa wafuasi wao, hii itawasaidia watu ambao wanashambuliwa zaidi kuweza kuweka picha zao katika mtandao huu bila ya kuwa na hofu ya kushambuliwa na watu ambao wanamsimamo tofauti.

Instagram inasema kwamba lengo ni kuufanya mtandao huu wa kirafiki na sehemu ya kufurahia na zaidi mtandao huu unataka uwe ndio sehemu salama kwa watu kueleza maoni yao.

SOMA PIA:  Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake #Uchambuzi

Huduma hii imeanza kwa watumiaji ambao wanapata maoni mengi zaidi katika picha zao na pengine kwa wakati fulani itawafikia watumiaji wote.

Teknokona tunapinga matusi na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamiii ambayo ni kinyume cha sheria za nchi, tunawashauri watumiaji wote kutumia mitandao hii huku wakiweka heshima na maadili mbele.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com