iOS10: kuja na mabadiliko kadhaa! #Apple #iOS

0
Sambaza

Miezi kadhaa kabla ya iOS10 kuachiwa na apple tayari baadhi ya mabadiliko ambayo inategemewa kuyaleta yameanza kujadiliwa na mitandao mbali mbali, pamoja na kuja na emoji mpya zipatazo miamoja pia OS hii itafanyiwa mabadiliko katika muonekano wa baadhi ya vitu huku baadhi ya app pia zikiwa zimepewa mabadiliko.

Apple wanatarajia kuachia toleo lao la kumi la OS ya vifaa vyao kama iPhone na iPad, ingawa toleo hili litawafikia watumiaji baadaye mwezi Septemba lakini zipo taarifa za baadhi ya mabadiliko hayo na makala hii itaangazia baadhi ya mabadiliko ambayo kimsingi yatawagusa watumiaji wengi wa Afrika mashariki.

SOMA PIA:  Daisy: Roboti wa Apple anayefumua simu 200 ndani ya lisaa

1.Emoji.

Apple wameleta walau emoji mpya 100 ambazo kwa wingi ni kwaajiri ya kuongeza utofauti wa rangi za emoji kwaajiri ya watu wa asili ama jinsia mbalimbali. Zaidi apple wameingia katika vichwa vingi vya habari baada ya kubadili emoji ya bastola na kuleta emoji ya kanyaboya la bastola.

ios10

Baadhi ya emoji zilizoongezwa. Picha na mtandao

2.App ya Ujumbe.

Apple wameifanyia mabadiliko app hii ili kuipa mvuto zaidi kwa watumiaji, imeongezewa uwezo wa kutuma note pamoja na uwezo wa kutuma link zikiwa na muhutasari wa kilichomo ndani kiujumla hapa pana mabadiliko mengi ingawa sio ukiwa unamtumia mtumiaji wa android basi ataona maandishi tu hivyo vingine ni lazima mpokea ujumbe atumie pia apple.

iOS10

Sasa watumiaji wa iPhone wataweza kushirikishana note zilizoandikwa kwa mkono.

3. Lock screen.

Hapa pamefanyiwa pia mabadiliko makubwa na kubadilisha namna iPhone imezoeleka, watumiaji sasa wataweza kufanya mambo mengi kabla hata ya kuifungua simu. Kwa utaratibu mpya mtumiaji anaweza kuangalia kalenda ama kuangalia taarifa mbalimbali za app kupita Notisification ambayo kwa sasa imekuwa shirikishi zaidi.

ios10

Muonekano mpya katika lock screen

4. Mabadiliko mengine.

Yapo mabadiliko mengine katika iOS10 kama katika app za Ramani Apple music na pia mabadiliko ya kimuundo katika control centre ya simu, mabadiliko haya yatawafikia watumiaji wa kawaida mwezi wa tisa hivyo kwa sasa bado yanafanyiwa marekebisho na maboresho zaidi.

SOMA PIA:  Namna ya kurudisha picha/video ulizovifuta kwenye simu za Android/iOS #Maujanja

Teknokona inaendelea kukuletea habari mbali mbali za teknolojia kwa lugha ya Kiswahili tembelea kurasa zetu za Facebook Twitter na Instagram kwa jina la @teknokona.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com