iOS 9.3 yasababisha kasheshe kwa vifaa vya zamani

0
Sambaza

Apple walitoa toleo jipya la iOS 9.3 tarehe 21 mwezi wa tatu, toleo hilo linatakiwa liwekwe kwenye iPhones na iPads zote ili ziweze kupata vipengele vipya ambavyo vimeongezwa. Lakini katika hali isiyo ya kawaida iPhones na iPads za zamani zimepatwa na kasheshe baada ya kuwekewa OS hii mpya.

iOS 9.3 -Update

Apple wa walileta iOS 9.3 wiki iliyopita ikiwa imesheheni vipengele vipya vingi ambavyo havikuwepo katika toleo lililopiata, toleo hili lilipata mrejesho mzuri kwa ujumla kutoka kwa mitandao mingi ambayo ililifanyia uchambuzi na pengine hili lilisababisha watumiaji wengi zaidi kushusha kuweka katika simu ama iPad zao.

SOMA PIA:  Mauzo ya bidhaa za Apple zenye rangi nyekundu

Imeripotiwa kwamba baadhi ya iPhones na iPads za baadhi ya watumiaji zilipatwa na shida baada ya update hii na shida hiyo ilivifanya vifaa hivi kutoweza kutumika kwa muda fulani.

Ripoti zinasema kwamba waliolalamika zaidi ni wamiliki wa vifaa vya zamani ambavyo havina uwezo wa kusoma fingerprints na wao ili kukamiliasha zoezi la update walitakiwa kuwa wanakumbuka taarifa za akaunti iliyotumika kuandikisha kifaa husika kwa mara ya kwanza kabisa kitu ambacho sio watu wote wanacho hasa ukizingatia kwamba wengine wanamiliki vifaa ambavyo walivinunua kama mtumba. Hii ilisababisha watumiaji hao kushindwa kutumia vifaa vyao kwa muda kwa kukosa taarifa hizo.

SOMA PIA:  Hatimaye mwanzilishi wa Android azindua simu yake ya Essential

Apple wamekwisha toa toleo jingine la OS hiyo ilikukabiliana na tatizo hilo na pia wametoa maelezo katika ukurasa wao jinsi ya kutatu atatizo hilo, na miongoni mwa njia ambazo walizitoa ni kutmia kompyuta yenye iTunes ama Mac kuupdate kifaaa chako ama kuondoa iCLOUD activation katika mtandao ili isisumbue ukiwa unaupdate.

Apple wanasema kama njia zilizowekwa hapo juu hazijakusaidia basi unatakiwa uwasiliane na Apple kwa msaada zaidi.

Matumaini yetu kwamba njia ambazo Apple wamezitoa zitakusaidia kutatua shida yako kama wewe ni mmoja ya watu ambao walipatwa na kasheshe hilo.

Vyanzo: The independent na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com