iPhone 6 yamlipukia na kumuunguza mtu

1
Sambaza

Mwanaume mmoja nchini Australia ameumia vibaya baada ya betri la simu yake ya iPhone 6 kulipuka na kushika moto.

Bwana Clear akionesha jeraha hilo

Bwana Gareth Clear mwenye umri wa miaka 36 amewasihi Apple kuwapa taarifa watumiaji wake juu ya hatari za milipuko ya betri zilizo kwenye simu zake.

Utengenezaji wa simu zilizonyembamba zaidi ndio unazidi kuleta hatari katika utengenezaji wa mabetri yake

Tukio lilitokeaje?

Inasemekana alikuwa akiendesha baiskeli wikiendi hii na huku simu hiyo ikiwa kwenye mfuko wa nyuma wa kaptula yake aliyokuwa ameivaa. Alidondoka na baiskeli yake na ghafla akaanza kushuhudia moshi ukitoka katika eneo la mfuko uliokuwa na simu hiyo.

SOMA PIA:  Chip mpya ya Qualcomm: Simu za bei nafuu (Featured phones) kuja na uwezo wa 4G LTE

Inasemekana kilichotokea ni kutokana na simu hiyo kugonga chini na hivyo sehemu zisizotakiwa kugusana ndani ya betri la simu hiyo zikagusana na hivyo kusababisha mlipuko.

Simu hiyo; Utengenezaji wa simu zilizonyembamba zaidi ndio unazidi kuleta hatari katika utengenezaji wa mabetri yake

Mabetri aina ya lithium ion ambayo ndiyo yanatumika sana katika simu yana hatari za mlipuko hasa pale ambapo yakigongwa.

Tawi la Apple la nchini Australia lilimtafuta Bwana huyo Clear na kumsaidia gharama za matibabu na utaratibu wa kumpatia simu nyingine.

SOMA PIA:  Youtube yazidi kuwawekea ngumu wenye msimamo mkali

Soma Pia – Ukiona haya, Fahamu muda wa Kubadilisha Betri la simu yako umefika!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com