iPhone Ikiwa Inaendeshwa Na OS Ya Android!

0
Sambaza

Unaweza ukachukulia ni kama kituko, hata mimi nlivyoona mara ya kwanza nlishangaa. Lakini pia ndio kawaida ya Teknolojia huwa zinatushangaza.

Baada ya watu kujiuliza sana na mabishano mengi yakatolea hatimaye wataalamu wakakaa chini na kuja na mbinu ambayo itawezesha simu za iPhone kuweza kutumia programu endeshaji ya Android.

Kava Hilo Likiwa Linaendesha iPhone Kwa Kutumia Android OS

Kava Hilo Likiwa Linaendesha iPhone Kwa Kutumia Android OS

Jambo hili kwa jicho la karibu linaonekana kabisa kuwa haliwezekani, lakini cha kushangaza ni kwamba mwanzoni mwa mwaka huu kuna mtaalamu (Nick Lee) amegundua njia. Njia hii ni kwa kutumi kava la nje la simu.

SOMA PIA:  Post Picha Moja Instagram Ikiwa Imegawanyika Katika Vipande Tisa (9)! #Android #iOs

Yaani kava hilo litakuwa na programu endeshaji ya Android. Kava hilo litakuwa lina OS ya Android Marshmallow ndani yake ambayo imeboreshwa kidogo ambalo pia litahusisha na App ili kuwezesha simu ya iPhone kuwaka kwa kutumia OS ya Android.

Utambulisho Wa MESUIT Case

Utambulisho Wa MESUIT Case

Ukiachana na bwana Lee, kampuni kutoka huko china, Haimawan imeamua kupeleka teknolojia hii mbele zaidi. Yenyewe imekuja na wazo kama la bwana Lee – kuwa na kava la simu lenye programu endeshaji ya Android – lakini likiwa na maboresho kidogo.

SOMA PIA:  Mambo 10 ya ujanja ujanja unayoweza kufanya kwenye iPhone 6/iPhone 6+

Kava hilo linaitwa MESUIT Case, ndani yake lini hardware ambayo inaendeshwa na Android OS. MESUIT Case pia inakuja ikiwa imeambatana na betri na pia kava hilo linakuja na GB 16 za ujazo. Bado hawakuishia hapo pia ina lina sehemu ya kuingizia laini nyingine (zile ndogo kabisa) na hii ni ili kurahisisha kutumika katika OS ya Android.

MESUIT Case

MESUIT Case

MESUIT Case inakosa vitu vidogo kama vile sehemu ya HDMI, Memori Kadi (SD Card) na sehemu ya USB, kumbuka kava la Lee halikuwa kwa ajili ya kuuza, lakini hili la MESUIT ni kwa ajili ya soko. Linaanza kupatikana kwa dola 150 za kimarekani huko nchini china

SOMA PIA:  Twitter Lite yaanza kupatikana katika baaadhi ya nchi

Niandikie sehemu ya comment hapo chini je wewe ungependa simu yako itumie OS nyingine tofauti na ile iliyokuja katika simu yako? Ningependa kusikia kutoka kwako

Tembelea TeknoKona kila siku ili uwe karibu na habari na mambo mbalimbali yanayohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com