Mtumiaji wa iPhone: Njia hii Haitasaidia Kutunza chaji yako - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtumiaji wa iPhone: Njia hii Haitasaidia Kutunza chaji yako

0
Sambaza

Kwa muda mrefu kumekuwa na imani kwamba moja ya njia ya kutunza chaji ya simu yako ni kwa kuhakikisha kwamba hakuna app ambazo zinafanya kazi na wewe hauzitumii, hi ni kweli lakini ni  kwa watumiaji wa Android tuu na sio watumiaji wa iPhone.

source site

source link Imani kwamba ukifunga app ambazo zinajiendesha katika background ya simu yako imekuwapo kwa muda mrefu sasa na ni watumiaji wengi sana wa simu zote zikiwamo iPhone wamekuwa wakiitumia njia  katika harakati za kupunguza matumizi ya chaji za simu zao.iphone chaji

Mwanzoni mwa wiki hii mtumiaji mmoja wa iPhone aliamua kumuandikia Mtendaji mkuu wa Apple bwana Tim Cook na kumuuliza juu ya swala hilo, bosi huyo wa Apple hakujibu swali hili lakini makamu wa raisi wa uhandisi wa software alilijibu swali hilo.

INAYOHUSIANA  Kodi kwenye mitandao ya kijamii yaanza rasmi Uganda

Mtumiaji huyo aliuliza iwapo Tim Cook huwa anafunga app zilizo katika background na iwapo zoezi hilo linasaidia katika uhifadhi wa chaji ya betri, swali hilo lilijibiwa na makamu wa raisi wa uhandisi wa software kwamba hapana na hapana yaani bosi huyo alisema kwamba huwa hafungi app zilizo katika background na pia kufunga hakusaidii uhifadhi wa chaji ya simu.

njia ya kuzima app haisaidii kuhifadhi chaji kwa iphone

Picha ya barua pepe aliyoandika mteja wa Apple pamoja na majibu yake.

source url Majibu hayo ya ni ya kuaminika na kwa ujumla yameondoa tetesi zote tulizokuwa tunazijua ama kuzisikia juu ya kuzima app zinazofanya kazi katika background.

Kuanzia sasa watumiaji wa simu za iPhone watatumia ‘multitasking‘ ambayo ndiyo inamfanya mtumiaji kuweza kutumia app moja wakati nyingine inaendeea kufanya kazi bila wasi wasi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.