iPhone X yabainika kuwa na tatizo kwenye uwanja wa kuandikia sms

1
Sambaza

iPhone X ni ya simu janja mpya kutoka Apple ambayo tayari imeshaanza kupatikana duniani kote na imeonekana watu wengi kujitokeza kununua simu hiyo au hata kwa kuagiza lakini tangu Nov, 3 2017 kuna tatizo limebainishwa kwenye simu hiyo na kukera watumiaji wake.

Mawasiliano kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno ni njia mojawapo maarufu sana iliyodumu kwa miongo kadhaa na mpaka hivi wa leo njia hiyo ya mawasiliano bado inatumika na wala haitegemei kukoma. Wateja walionunua iPhone X siku kadhaa zilizopita wamejikuta katika wakati mgumu pale wapipokuwa wakitaka kuandika herufi “i” na badala yake kubadilika na kutokea herufi “A” ikifuatiwa na alama ya kiulizo (⍰).

Kiufundi tatizo hilo limefahamika kama Variation Selector 16 (VS-16) ambayo ni kipande cha programu ambayo kazi yake inaunganisha kwa pamoja herufi mbili na emoji lakini badala yake kipande hicho cha programu kina makosa na majibu yake inaonyesha herufi “A” pamoja na “⍰”. Huku watumiaji wengi wakiripoti kuwa wanaona inatokea “!” na “⍰” pale wanapoanza andika neno linaloanzia na herifi “i”.

Adha inayotokea pale mtu anapotaka kuandika neno linaloanzia na herufi ‘i’. Tatizo hili limeathiri watumiaji wa bidhaa za Apple zinazotumia iOS 11.1.

Suluhisho la tatizo.

Mpaka sasa hakuna suluhisho la kudumu lilitolewa ingawa Apple imetoa mbninu fulani ya kuweza kuandika herufi “i” bila kubadilika na kuandika kitu kichoeleweka. Unaingia  settings > general > keyboard > text replacement kisha unabofya kwenye alama ya “+”. Kwa upande wa phrase weka herufi “I” na kwa upande wa shortcut weka herufi “i”.

SOMA PIA:  Simu janja chini ya nusu ya asilimia moja ndio zinatumia Oreo #Ripoti

Tayari Apple wanafanyia majaribio (beta) toleo la iOS 11.2 na watumiaji wa Apple wanatumaini Apple wameweza kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo kabla ya toleo la iOS 11.2 kuanza kupatikana kwa wote.

Vyanzo; Telegraph, Inverse, Independent

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com