Jacquard: Jaketi janja kutoka Google na Levi’s

0
Sambaza

Google na kampuni nguli ya ubunifu wa mavazi, Levi’s, kwa kushirikiana pamoja wameleta jaketi janja linalofahamika kwa jina la Jacquard.

Nguo janja Jacquard

Teknolojia hii inahusisha vifaa vidogo vidogo vya elektroniki vinavyoshonewa kwenye kitambaa cha nguo (eneo flani), kimkanda kidogo kinachovalishwa kwenye nguo pia, simu yako ya mkononi pamoja na app inayofanya muunganisho wa mawasiliano kati ya simu yako na nguo.

koti nguo google teknolojia

Jaketi hili lina teknolojia ndogo ndogo za elektroniki ndani ya kitambaa chake na kifaa kingine cha nje na hivyo kumuwezesha mvaaji kuweza kuchukua hatua mbalimbali zinazohusisha simu yake moja kwa moja kwa kushika sehemu flani za koti hilo.

SOMA PIA:  Instagram Yaja Na 'Sticker' Kama Snapchat!

Teknolojia gani hasa inaunganisha koti na simu yako?

Koti linakuja na teknolojia ya Bluetooth na hivyo mvaaji inabidi aunganishe mawasiliano ya kati ya simu na koti hili. Mfano kama mtumiaji anataka kuanzisha mziko kucheza au kuusimamisha (pause) basi anaweza kugusa mara mbili eneo flani la koti hili na hicho kitafanyika moja kwa moja.

Google Jacquard

Teknolojia imetengenezwa na Google pamoja na Levi’s chini ya ‘Project’ waliyoipa jina la Jacquard

Vingine utakavyoweza kufanya kupitia koti la Jacquard;

  • Kupokea simu
  • Mambo yote muhimu yanayohusisha apps za kusikiliza muziki
  • Kupata maelekezo ya mahali (directions) etc
SOMA PIA:  Alphabet yapeleka WiFi Puerto Rico kwa mfumo wa maputo yanayopaa

Hizi ni teknolojia ambazo kawaida ungeziona kwenye filamu ila Google wakishirikiana na Levi’s wanaonesha ni jambo linalowezekana na tulitegemee sana tuu katika miaka inayokuja.

Kutakuwa na kataa chochote kanakowaka?

Hapana, kampuni ya Levi’s imesema wateja wa nguo zao ni watu ambao wasingependa kuvaa nguo ya namna hiyo – yenye vijitaa taa. Na hivyo teknolojia iliyotumika ndio maana imekuwa ndogo sana kiasi cha kutosha kushonewa ndani ya mavazi haya – kwa kuanzia ni makoti. Eneo pekee litakalokuwa linauwezo wa kubadilika rangi kulingana na kinachoendelea kwenye simu yako ni kimkanda kidogo ambacho kinauwezo wa kuvishwa na kuondolewa kwenye nguo.

SOMA PIA:  Google waliuza simu za Pixel takribani milioni 4 mwaka 2017

Kimkanda hichi peke yake akiwezi kufanya kazi, kinategemea teknolojia iliyokwenye nguo.

Utaweza kuliosha?

Kuna kidude kidogo kitakachokuja pia na nguo hiyo kinachochomekwa kitakuwa na uwezo wa kuondolewa kutoka kwenye nguo yako. Pale utakapoondoa kipande kidogo sehemu zingine zote za nguo utaweza kufua bila tatizo.

Bei?

Makoti ya Jacquard yataanza kupatikana kipindi flani mwaka huu (Mwezi wa tisa – kumi) na bei ya takribani laki 7 (USD 350).

Je una mtazamo gani juu ya teknolojia ya namna? Je unadhani ina nafasi ya kuwa maarufu na kupata soko la uhakika?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com