Je, E-Cigarettes Ni Salama? Hiki Ndicho Kinachojulikana. - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Je, E-Cigarettes Ni Salama? Hiki Ndicho Kinachojulikana.

0
Sambaza

Kila mtu ana lake la kusema kuhusu Sigara za umeme (E-Cigarettes): Waulize watu 10 kuhusu usalama wake na utapata majibu 10 tofauti. Pengine hata ubishi mkubwa unaweza kuzuka kwani hakuna taarifa za kutosha za kitafiti za kuzima ubishi kwa sasa. Hata-hivyo, kuna vitu vichache ambavyo wataalamu wanakubaliana.

5185Uvutaji wa mvuke wa sigara za umeme ni kitu chenye utata. Hii ni kwa sababu uvutaji huu ni kitu kipya na utata wake una sura mbili: Kwanza, sayansi ya kujua usalama wake haijatambulika bado. Na ya pili, ambayo labda ni muhimu zaidi, ni kwamba pande za kisiasa na za kibiashara bado hazijagundua wapi pa kuegemea kukidhi maslahi yao. Katika biashara: Je, kampuni kubwa za biashara ya tumbaku zinaonaje uvutaji huu mpya – kama ushindani au fursa mpya? Katika siasa: Je, uvutaji wa e-cigarettes ni mwanzo mpya kwa afya bora kwa jamii au ni sigara nyingine mbadala (yani matatizo ya afya yakibaki palepale)?Swahili Version

Kwa maswali haya na mengine yasiyokuwa na majibu bado, hatuwezi kutoa jibu la ndio au hapana kama e-cigarettes ni salama katika makala moja ya Teknokona. Tunachoweza kufanya ni kuangalia ushahidi suala hili kwa kuzingatia maswali mawili muhimu na kukuambia maoni  ya wataalamu juu ya yale yanayojulikana kuhusu uvutaji wa e-cigarettes kwa sasa.

Je, E-Cigarettes Zina Vitu Hatarishi?

Tuanze na kisichokuwa na ubishi: Nikotini (‘Nicotine’) ipo kwenye e-cigarettes nyingi. Uwepo wa Nikotini ndiyo maana nzima tunapozungmzia e-cigarettes kuwa mbadala wa sigara za tumbaku. Ingawa fleva mbalimbali zinatajwa kupamba sigara hizi mpya kwenye vyombo vya habari, e-cigarettes zinazouzwa zaidi kwenye maduka ya kawaida ni zile zisizokuwa na fleva au zenye menthol na huku zikiwa na Nikotini ya kutosha.

Nikotini ni kitu kinachompa mtu hamu ya kuvuta, lakini hakileti saratani. Jambo hili linafanya wanaotetea e-cigarettes kusema kwamba “Tatizo la sigara za kawaida ni vitu vya ziada, moshi na kemikali, na siyo Nikotini,” Kitu ambacho si kweli. Nikotini ina matatizo yake yenyewe. Nikotini inaweza kuathiri akili ya kijana wa chini ya miaka 20, na siyo salama kwa wanawake wenye mimba: Nikotini ina-ingiliana na ukuaji wa mtoto akiwa tumboni mwa mama, ikiwa pamoja na matatizo ya ukuaji wa mapafu, na inaweza kusababisha kuzaa kabla ya muda unaopaswa kuzaa.

Visababishi vya Saratani, vinapatikana ndani ya tar, ambayo ni moja ya vitu vinavyopatikana kwenye sigara ya kawaida. Sigara za umeme hazina tar, kwa-hiyo faida mojawapo ya kuvuta sigara hizi ni kwamba utakuwa unakosa hiki kisababishi cha saratani. Hatahivyo, kuna uwezekano ukawa unapata kemikali zingine zenye madhara kwako. Diacetyl, inayotumika kwenye fleva nyingi, ni salama kwa kula ila siyo kwa kuivuta. Panya waliojaribiwa kwa kuwapa mvuke wa sigara za umeme walipata madhara madogo ya mapafu, lakini ni madogo zaidi ya madhara ambayo wangepata kwa moshi wa sigara ya kawaida. Na katika tafiti ambayo imeripotiwa sana, watafiti waligundua kwamba e-cigarettes huweza kutunga formaldehyde zaidi ya sigara za tumbaku, iwapo kama joto linaloipa sigara hizo moto likizidi nguvu kufikia kiasi kisicho cha kawaida. Wakati kuvuta mvuke wa sigara za umeme si salama kama kuvuta pumzi ya hewa ya kwaida, ni bora zaidi ya kuvuta sigara za kawaida.

Je, hii inatosha kupigia mstari kwamba e-cigaretts haina madhara?

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization) halina mtazamo chanya, ulio na uhakika, wanapoelezea kuhusu mambo yasiyojulikana kuhusu madhara ya e-cigarettes:

“Hatari zinazowezekana kuwepo kwa afya za watumiaji [wa e-cigarettes] hazijulikani. Zaidi, majaribio ya kisayansi yanaonesha kwamba bidhaa zinatofautiana sana kwenye kiwango cha nikotini na kemikali nyingine zinazowekwa na hakuna njia za watumiaji kujua kwa uhakika nini kilichopo ndani ya bidhaa hizo wanazonunua.”

Kwa maneno mengine, tatizo hili linafanana na la usambazaji wa bidhaa za virutubishi: Hakuna ulazima wa kuhakiki ni nini haswa na kwa kiasi gani kilichopo ndani ya virutubishi vinavyouzwa na watu wengi kama tiba mbadala.

Kuna hatari nyingine isiyokuwa kwenye mvuke wenyewe: Vijazio vinakuwa na nikotini nyingi inayoweza kuvutwa, kumezwa, au kupitia kwenye mwili. Kunywa majimaji yatokayo vijazio hivi tayari yameua mtoto mmoja. Ukitumia majimaji hayo, tumia kwa umakini na weke mbali na watoto au wanyama wako.

Je, Uvutaji wa E-Cigarettes Utakusaidia kuacha Kuvuta?

Kwa kuwa e-cigarettes zina vitu vyenye madhara madogo kuliko sigara za tumbaku, inaingia akilini kwamba ni vyema zaidi kiafya kutumia hizo na kuachana na za tumbaku. Kama hilo ni kweli, wanasayansi wanaonekana kupata wakati mgumu kulidhibitisha hilo. Shirikisho la Mapafu Marekani (The American Lung Association),  “wana wasi-wasi na uvumi” unaosema kwamba e-cigarettes zinaweza kusaidia watu kuacha sigara za tumbaku; wanasema sayansi ya kuthibitisha hilo haijagundulika bado.

Kwa mfano tafiti hii,iliyochapwa kwenye JAMA Internal Medicine mwaka jana. Ya wavuta tumbaku wakipiga simu kuomba msaada wa kuacha, wale waliotumia e-cigarettes walikuwa hawana muelekeo wa kuacha baada ya kufanya hivyo. Waandishi wa tafiti hiyo wanaandika kwamba, inawezekana kuvuta e-cigarettes inasaidia watu kuachana na sigara za tumbaku, ila kwa asilimia ndogo sana kiasi kwamba tafiti yao haikuweza kuiona.

Kwa upande mwingine, tafiti iliyochapwa kwenye jarida la Addiction iligundua kwamba wavutaji waliotumia e-cigarettes walikuwa na uwezekano wa asilimia 60% zaidi ya kufanikiwa kuacha zaidi ya wale waliotumia njia nyingine za kujipa nikotini. Kwa nini huu mkingano? Hili haliko wazi. Wavutaji hawa walikuwa na juhudi za kibinafsi za kuacha kuvuta, sio kwa kutafuta msaada kwa simu, na pia kuna uwezekano wa kuwepo sababu zingine muhimu za kutofautisha tafiti hizi mbili.

Tafiti mpya zaidi inaonesha mtazamo mwingine: watafiti wanaripoti kwenye jarida liitwalo the American Journal of Public Health kwamba—bila kuangalia wanaoacha, ila kwa kuwaangalia wale wanaovuta kwa mazoea -, wale waliojaribu e-cigarettes walikuwa na uwezekano mdogo zaidi wa kuacha uvutaji. Kwa maneno mengine, wanaovuta mvuke wa sigara za umeme huenda hawataki kuacha kabisa kuvuta.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba wamegundua wamepunguza madhara wanaojipatia mwilini na hivyo, kuvuta kiasi kidogo cha sigara za tumbaku na kuvuta e-cigarettes ni bora kuliko tabia waliozoea ya kuvuta sigara za tumbaku kwa wingi. Ila bila tafiti zaidi juu ya kwa nini wanafanya hivi, hatuna uhakika wa kusema ni kwa nini suala hili ni kama lilivyo hapaMafanikio ya kuachana na uvutaji yanaweza kutegemea na mambo kadhaa, kama dozi ya nikotini unayopata kwenye e-cigarette au ni kwa mara ngapi unaitumia. Hakuna muongozo amabao uliokubaliwa kwa kiasi cha uvutaji wa sigara za umeme kwa ajili ya kusaidia kuacha uvutaji. Hii inamaanisha kwamba hatujui badoo kama inasaidia watu kuacha uvutaji wa sigara za tumbaku au la, na hatuwezi kusema jinsi gani zinaweza kutumika kukusaidia wewe kuacha kuvuta sigara za tumbaku kama hilo ndilo lengo lako.

Je Makampuni Makubwa ya Tumbaku yanaipa ‘tafu’ umaarufu wa E-Cigarettes?

Makampuni ya sigara za tumbaku yako katika wakati wa usioeleweka katika hili suala: Wangependa sehemu hii ya soko ambayo inawapa sababu ya watu kuenedelea na uvutaji, ila pia wangependa soko lao lenye faida kubwa la tumbaku liendelee kuwepo.

Matokeo yake ni vita ya kiaina kati ya aina mbili za watengenezaji. Katika kundi moja, tuna kampuni huru zinazouza vyombo vya kujazia e-cigarettes zinazokutangazia ujaze fleva mbalimbali. Na kwa upande mwingine, watengenezaji wa e-cigarette zinazofanana na ‘cigar’ ambazo unaweza kuzitupa – sio za kujalizia na huwa na fleva ya sigara za tumbaku. Watengenezaji wakubwa wa aina hii ni Blu, ambao wanamilikwa na kampuni ya tumbaku.

Kampuni kubwa za tumbaku zinaonekana kuweka mategemeo yao kwa njia mbili: Kuuza vitu vinavyofanana na sigara ya tumbaku zikiwa na lebo zenye maonyo makubwa zaidi ya sigara za tumbaku, huku wakiandikia mamlaka ya chakula marekani kwamba washindani wao ‘huria’ ni hatari na wanahitaji kuchunguzwa zaidi.

Wakati huohuo, wauzaji huria wa e-cigarettes wanaonekana kuwa na nguvu kwenye soko lao. Wakati hilo soko likiwa linakuwa , ni muhimu kwa sisi watu wa kawaida kutilia maanani sayansi zaidi, na sio ushabiki.

Chanzo, Picha: Lifehacker Vitals

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply