Je iPhone 6 plus Yako Inatoa Picha Mbaya? Apple Waleta Programu Ya iSight Kwa Ajili Yako!

0
Sambaza

Watumiaji wa simu za Apple ambao wanatumia iPhone 6 Plus ambazo zina matatizo ya kamera yaani kamera inakua inatoa picha zenye ukungu (blurry) kidogo. Kama matatizo hayo yanakukumba huu unaweza ukawa ndio msaada juu ya simu yako hiyo.

Apple wameanzisha programu mahususi inayoitwa ‘iSight Camera Replacement Program’ baada ya kampuni kuona kuwa kuna baadhi ya simu ambazo walizalisha zenye matatizo hayo ya kamera. Matatizo hayo yanafanya picha ambazo zimepigwa na baadhi ya iPhone 6 plus kutokuwa na hadhi inayostahili.

Baadhi ya simu hizo ni zile zenye namba za utambuzi (serial number) ambao zilitengenezwa katika mwezi septemba 2014 mpaka januari 2015

iPhone_6_PLUS

Moja Kati Ya iPhone 6 Plus Inayotoa Picha Zenye Ukungu

Watumiaji ambao wame(na)kutana na matatizo haya  inawabidi waingie hapa  katika mtandao maalumu ambao umejikita katika kutatau tatizo hilo la simu za iPhone 6 Plus katika kamera ambazo zinatoa ukungu (blurry) katika kupiga picha

SOMA PIA:  Matumizi ya simu jela: Simu 13,000 zakamatwa Uingereza

Katika mtandao huo watumiaji wa iPhone 6 plus hizo wanaweza ingiza namba za utambulisho wa simu zao (serial number) ili kutambua kama simu zao zipo katiki zile simu ambazo zina matatizo hayo (zile za septemba 2014 mpaka januari 2015). Apple wamesema kama mtumiaji wa simu hiyo anataka kujiunga na programu hii basi simu yake (iPhone 6 Plus) inabidi iwe katika hali ya kufanya kazi yaani isiwe mbovu. Kama serial namba ya simu ipo katika zile za kati ya septemba na januari basi kampuni ya apple litafanya marekebisho ya kamera hiyo  bure

SOMA PIA:  Bill Gates asema anatumia simu ya Android, Ni samsung Galaxy S8?

Watumiaji wa simu ambao watajikuta namba za utambulisho wa simu zao zippo katika pprogramu hiyo itawabidi wachague namba ambavyo simu zao zinaweza kutegenezwa kamera katika machaguo matatu. chaguo la kwanza ni Kuipeleka simu hiyo kwa mtoa huduma aliethibitishwa na Apple, Chagua la pili ni kupanga muda wa kuonana (Appointment) na duka la mauzo la Apple na chaguo la tatu (la Mwisho)  ni Kuwasiliana na Apple kitengo cha ufundi mwenye simu aweze kuelezewa jinsi amabavyo kamera hiyo inavyowezwa kurekebishwa.

Apple pia wameweka wazi kuwa kabla ya mtu kutuma simu yake ikafanyiwe marekebisho hayo basi hana budi ku back up taarifa zake zote katika kompyuta yake kisha ndio aitume

SOMA PIA:  Mwanamke kulipa faini kutokana na kuchati wakati akiwa sinema

Pia Kwa wale ambao iPhone 6 plus zao zina matatizo kama vile ya kioo kupata nyufa inabadi warekebishe kwanza matatizo hayo kabla ya kutuma simu zao au kama wakiamua kutuma hivyo hivyo kutakua na gharama za ziada ili kuwezesha kutengeneza kwa vioo hivyoo

Kama hili linakuhusu, hutakiwi kupuuzia. Mwambie na mwenzio huwezi juu unaweza fufua kamera yake (hah!) Tuandikie unaonaje huduma za Apple? je wanajiweka karibu sana na wateja wao au ni mbinu tuu za kibiashara? Tuambie sehemu ya comment hapo chini.Pia usiache kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com